The Chanzo (@TheChanzo) header
The Chanzo (@TheChanzo) profile picture

We Are Bilingual Multimedia Storytellers Looking At The World From Ground Up. Una habari? WhatsApp/Telegram 0753815105

Dar es Salaam, Tanzania
Joined August 2020
Photo by The Chanzo (@TheChanzo)Photo by The Chanzo (@TheChanzo)Photo by The Chanzo (@TheChanzo)Photo by The Chanzo (@TheChanzo)Photo by The Chanzo (@TheChanzo)Photo by The Chanzo (@TheChanzo)Photo by The Chanzo (@TheChanzo)Photo by The Chanzo (@TheChanzo)Photo by The Chanzo (@TheChanzo)Photo by The Chanzo (@TheChanzo)
Yes, in My Lifetime: Haroub Othman na Suala la Zanzibar Ndani ya Muungano Tazama mapitio ya kitabu cha 'Yes, In My Lifetime: Selected works of Haroub Othman' hapa>youtu.be/SRIn4fmqjms
5
16
1,082
Chalamila: Wanafunzi wa vyuo waliokosa mikopo wafike Viwanja vya Posta Kijitonyama Novemba 14.
3
5
1
44
3,260
Chalamila apigilia msumari suala la kata 10 Temeke kutengwa kwa ajili ya shughuli za bandari.
11
9
3
116
12,534
Tundu Lissu Ahukumiwa Miaka Minne Jela Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam imemhukumu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu miaka minne gerezani kwa kosa la uchochezi. Hukumu hiyo iliyotolewa leo Novemba 06, 2026 na majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru imekuja baada ya Mahakama kueleza kuwa hakuna ushahidi wa kosa la uhaini aliloshitakiwa nalo, ambalo kutokana na ushahidi uliotolewa waliangalia kosa dogo lenye uhusiano na kosa la uhaini. Jaji Nduguru alieleza kuwa baada ya kupitia upya ushahidi kwa kuangalia kosa la uchochezi ilimkuta Lissu ana hatia. Upande wa Mashtaka ulipendekeza Lissu apewe adhabu kubwa inayohusisha kufingo cha miaka mitano, wakieleza kuwa makosa ya uchochezi yamekuwa mengi, huku wakitaja pia wakihusisha na matukio ya Oktoba 29. Lissu alitoa maoni yake kufuatia Mahakama kusema anamakosa ya uchochezi, na kusisitiza kuwa mashitaka dhidi yake ni ya kisiasa, na kwamba Majaji wamekuja na kosa jipya la uchochezi kutekeleza maelekezo ya kisiasa waliyopewa. Hata hivyo Lissu aliishauri Mahakama juu ya adhabu ya faini, akitaja kanuni za adhabu, lakini pia akigusia afya yake, na pia kufiwa. Hatimaye Mahakama ilitangaza hukumu yake kuwa ya miaka minne gerezani, na kueleza rufaa iko wazi.
1
5
15
1,774
Lissu: Tutafika tu.
1
82
1
350
14,165
The Chanzo tupo hapa Mahakama Kuu Masjala ya Dar es Salaam kukujuza kile kinachoendelea ambapo Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu atasomewa hukumu katika kesi ya uhaini inayomkabili.
11
42
2,190
Waandishi wambana kwa maswali Kamanda Muliro nje ya Mahakama
45
50
7
540
48,843
Namna Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu alivyofikishwa Mahakamani kwa ajili ya kusomewa hukumu ya kesi ya uhaini iliyokuwa inamkabili.
2
6
22
1,821
‘From vulnerability to opportunity’: Songwe’s inclusive boarding school for boys
3
12
1,459
Sakata la Tundu Lissu laibuka tena Umoja wa Mataifa, serikali yajibu Kushikiliwa kwa Tundu Lissu kumeibuka wakati wa majadiliano ya ripoti ya Tanzania ya haki za binadamu katika baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu leo Novemba 05, 2026. Hii ni baada ya mjumbe wa Uingereza kueleza kushikiliwa kwa Lissu kwa mujibu wa kikosi kazi cha UN, ni kushikiliwa kusikofuata sheria zinazokubalika. Hoja hiyo ilifanya Tanzania kutoa majibu ambapo ilisisitiza Mahakama isiwekewe siasa.
5
50
181
8,074
Serikali yasema inalaani matukio ya watu kutekwa na kupotezwa Tanzania Serikali ya Tanzania imesema inalaani matukio ya watu kutekwa na kupotezwa, haya yameelezwa leo Novemba 05, 2026, wakati serikali ya Tanzania ikijibu hoja mbalimbali zilizotolewa kuhusu ripoti yake ya haki za binadamu iliyowasilishwa na Waziri wa Katiba, Abdallah Ulega. Ripoti hiyo imetolewa leo, kwa ajili ya mapitio ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, ambapo Tanzania ni moja ya nchi zilizoridhia kufanya mapitio hayo ya mara kwa mara. Ripoti ya mwisho iliwasilishwa mwaka 2021, ikiwa ni ripoti ya tatu ya Tanzania.
28
45
4
131
12,518
Tanzania UN: Serikali yaeleza ripoti ya Chande haikuachiwa sababu ya kulinda ushahidi Akizungumza leo Novemba 05, 2026, wakati wa kutoa ripoti ya tathmini ya haki za binadamu Tanzania, katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, Waziri wa Katiba na Sheria, Abdallah Ulega, ameeleza sababu ya ripoti ya uchunguzi matukio ya Oktoba 29 kutokuwekwa wazi ni ili kulinda ushahidi. "Serikali inatambua shauku ya umma ya kuchapishwa kwa ripoti kamili. Hata hivyo, uwekaji wazi lazima upimwe dhidi ya uchunguzi unaoendelea na mashtaka yanayoweza kufunguliwa. Kuichapisha mapema kunaweza kuharibu ushahidi, kuhatarisha mashahidi au kuathiri haki ya kusikilizwa kwa haki na dhana ya kutokuwa na hatia," ameeleza Ulega.
7
8
2
27
4,748
Tanzania UN: Maamuzi ya Mahakama lazima yaheshimiwe hata kama hatukubaliani nayo Akizungumza leo Novemba 05, 2026, wakati wa kutoa ripoti ya tathmini ya haki za binadamu Tanzania, katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, Waziri wa Katiba na Sheria, Abdallah Ulega amesisitiza umuhimu wa kuheshimu maamuzi ya Mahakama, hata pale ambapo kuna kutokukubaliana nayo.
27
7
3
48
13,945