ROZARI TAKATIFU - MATENDO YA UCHUNGU (Jumanne na Ijumaa)
1. Yesu anatoka jasho la damu kwa ajili yetu.Tumwombe Mungu atujalie sikitiko la dhambi.
2. Yesu anapigwa kwa mijeledi kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuacha dhambi za uchafu.
3. Yesu anatiwa miiba kichwani kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kushinda kiburi.
4. Yesu anachukua Msalaba kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuvumilia taabu.
5. Yesu anakufa Msalabani. Tumwombe Mungu atujalie kuwapenda Yesu na Maria.
SALA YA ASUBUHI
+Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
Tuusifu Utatu Mtakatifu wa Mungu mmoja, sasa na siku zote na milele amina. Ee utatu Mtakatifu wa Mwenyezi Mungu; +Baba, +Mwana na +Roho Mtakatifu. Ninasadiki kuwa upo hapa na mahali pote.
Ee Mungu wangu, umeniumba, umenikomboa, umenifanya mkristu, umenizidishia neema zako, umenitayarishia makao yangu mbinguni.
Ee Mungu wangu, nakuabudu, nakushukuru, nakuomba toba, nakupenda. Ee Mungu wangu, ninakutolea roho yangu, na mawazo, na maneno, na kazi na furaha, na mateso yangu, uyapokee unipe neema yako nisitende leo dhambi, Amina.
BABA YETU.
Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
Utupe leo mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni. Amina.
SALAMU MARIA.
Salamu, Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe, umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu, mzao wa tumbo lako, amebarikiwa.
Maria mtakatifu, Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
KANUNI YA IMANI.
Nasadiki kwa Mungu, Baba Mwenyezi, Muumba wa mbingu na dunia; na kwa Yesu Kristo Mwanae pekee, Bwana wetu, aliyetungwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria, akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato, akasulubiwa, akafa, akazikwa, akashukia kuzimu; siku ya tatu akafufuka kutoka wafu, akapaa mbinguni; ameketi kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi; kutoka huko atakuja kuwahukumu walio hai na wafu.
Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Kanisa takatifu Katoliki, ushirika wa Watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili, na uzima wa milele. Amina.
AMRI ZA MUNGU.
1. Ndimi Bwana Mungu wako, usiabudu miungu wengine.
2. Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako.
3. Shika kitakatifu siku ya Mungu.
4. Waheshimu baba na mama; upate miaka mingi na heri duniani.
5. Usiue.
6. Usizini.
7. Usiibe.
8. Usiseme uongo.
9. Usitamani mwanamke asiye mke wako.
10. Usitamani mali ya mtu mwingine.
AMRI ZA KANISA.
1. Hudhuria Misa takatifu Dominika na Sikukuu zilizoamriwa.
2. Funga siku ya Jumatano ya Majivu; usile nyama siku ya Ijumaa Kuu.
3. Ungama dhambi zako walau mara moja kila mwaka.
4. Pokea Ekaristi Takatifu hasa wakati wa Pasaka.
5. Saidia Kanisa katoliki kwa zaka.
6. Shika sheria katoliki za ndoa.
Ee Maria Bikira Mtakatifu, Mama wa Mungu na Mama yangu, nawe Mtakatifu Yosefu, Nawe Malaika Mlinzi wangi, Nanyi watakatifu somo wangu, nanyi Watakatifu wote, Niombeeni nipate kuacha dhambi, nilindeni siku ya leo na siku zote, na saa ya kufa kwangu, Amina.
MALAIKA WA BWANA
•Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria, Naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
~Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria mtakatifu Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
•Ndimi mtumishi wa Bwana, Nitendewe ulivyonena.

•Neno wa Mungu akatwaa mwili, akakaa kwetu.

Utuombee Mzazi mtakatifu wa Mungu, tujaliwe ahadi za Kristo.
Tuombe:
Tunakuomba, ee Bwana, utie neema yako mioyoni mwetu, ili sisi tuliojua kwa maelezo ya Malaika kwamba Mwanao amejifanya mtu, kwa mateso na msalaba wake utufikishe kwenye utukufu wa ufufuko. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu Amina.
SALA KWA MALAIKA MLINZI
Malaika mlinzi wangu, unilinde katika hatari zote za roho na za mwili. Amina.
Moyo Mtakatifu wa Yesu, Utuombee
Roho za waamini marehemu wapate rehema kwa Mungu wapumzike kwa amani.

"Nimeshatenda dhambi moja ya mauti, basi ngoja niendelee kutenda nyingine. Mwisho wa wiki nitaenda kuungama zote pamoja."
Huu ni mtazamo hatari dhidi ya huruma ya Mungu (presumption). Ni kuhatarisha wokovu kwa makusudi: unaweza kufa kabla ya kupata nafasi ya kutubu na kupokea Sakramenti ya Kitubio. Pia, kuahirisha maungamo kwa makusudi kunatia mashaka juu ya unyofu wa moyo unaohitajika katika Kitubio.
Tusicheze na neema ya Mungu. Kutubu ni sasa.
ROZARI TAKATIFU, MATENDO YA FURAHA (Jumatatu na Jumamosi)
1. Malaika Gabrieli anampasha habari Maria kuwa atakuwa Mama wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie unyenyekevu.
2. Maria Mtakatifu anakwenda kumtembelea Elizabeti. Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya jirani.
3. Yesu anazaliwa Betlehemu. Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara.
4. Yesu anatolewa
hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo.
5. Maria anamkuta Yesu hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu.
Mungu akubariki na kukulinda.
Mungu akuangazie nuru za uso wake na kukufadhili.
Mungu akuinulie uso wake na kukupa amani!
SALA YA ASUBUHI
+Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
Tuusifu Utatu Mtakatifu wa Mungu mmoja, sasa na siku zote na milele amina. Ee utatu Mtakatifu wa Mwenyezi Mungu; +Baba, +Mwana na +Roho Mtakatifu. Ninasadiki kuwa upo hapa na mahali pote.
Ee Mungu wangu, umeniumba, umenikomboa, umenifanya mkristu, umenizidishia neema zako, umenitayarishia makao yangu mbinguni.
Ee Mungu wangu, nakuabudu, nakushukuru, nakuomba toba, nakupenda. Ee Mungu wangu, ninakutolea roho yangu, na mawazo, na maneno, na kazi na furaha, na mateso yangu, uyapokee unipe neema yako nisitende leo dhambi, Amina.
BABA YETU.
Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
Utupe leo mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni. Amina.
SALAMU MARIA.
Salamu, Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe, umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu, mzao wa tumbo lako, amebarikiwa.
Maria mtakatifu, Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
KANUNI YA IMANI.
Nasadiki kwa Mungu, Baba Mwenyezi, Muumba wa mbingu na dunia; na kwa Yesu Kristo Mwanae pekee, Bwana wetu, aliyetungwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria, akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato, akasulubiwa, akafa, akazikwa, akashukia kuzimu; siku ya tatu akafufuka kutoka wafu, akapaa mbinguni; ameketi kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi; kutoka huko atakuja kuwahukumu walio hai na wafu.
Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Kanisa takatifu Katoliki, ushirika wa Watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili, na uzima wa milele. Amina.
AMRI ZA MUNGU.
1. Ndimi Bwana Mungu wako, usiabudu miungu wengine.
2. Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako.
3. Shika kitakatifu siku ya Mungu.
4. Waheshimu baba na mama; upate miaka mingi na heri duniani.
5. Usiue.
6. Usizini.
7. Usiibe.
8. Usiseme uongo.
9. Usitamani mwanamke asiye mke wako.
10. Usitamani mali ya mtu mwingine.
AMRI ZA KANISA.
1. Hudhuria Misa takatifu Dominika na Sikukuu zilizoamriwa.
2. Funga siku ya Jumatano ya Majivu; usile nyama siku ya Ijumaa Kuu.
3. Ungama dhambi zako walau mara moja kila mwaka.
4. Pokea Ekaristi Takatifu hasa wakati wa Pasaka.
5. Saidia Kanisa katoliki kwa zaka.
6. Shika sheria katoliki za ndoa.
Ee Maria Bikira Mtakatifu, Mama wa Mungu na Mama yangu, nawe Mtakatifu Yosefu, Nawe Malaika Mlinzi wangi, Nanyi watakatifu somo wangu, nanyi Watakatifu wote, Niombeeni nipate kuacha dhambi, nilindeni siku ya leo na siku zote, na saa ya kufa kwangu, Amina.
MALAIKA WA BWANA
•Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria, Naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
~Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria mtakatifu Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
•Ndimi mtumishi wa Bwana, Nitendewe ulivyonena.
~Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria mtakatifu Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
•Neno wa Mungu akatwaa mwili, akakaa kwetu.
~Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria mtakatifu Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
Utuombee Mzazi mtakatifu wa Mungu, tujaliwe ahadi za Kristo.
Tuombe:
Tunakuomba, ee Bwana, utie neema yako mioyoni mwetu, ili sisi tuliojua kwa maelezo ya Malaika kwamba Mwanao amejifanya mtu, kwa mateso na msalaba wake utufikishe kwenye utukufu wa ufufuko. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu Amina.
SALA KWA MALAIKA MLINZI
Malaika mlinzi wangu, unilinde katika hatari zote za roho na za mwili. Amina.
Moyo Mtakatifu wa Yesu, Utuombee
Roho za waamini marehemu wapate rehema kwa Mungu wapumzike kwa amani.
+Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
Ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana. Mtakeni Bwana na nguvu zake, utafuteni uso wake siku zote. (Zab. 105:3-4)
Historia Mpya ya Muungano wa Kinga na amani baada ya Miaka 500.
Mambo yamebadilika sana katika historia ya Uhusiano kati ya Ufalme wa Uingereza na Kanisa Katoliki.
Karne tano (miaka 500) baada ya Mfalme Henry VIII kujitenga na Papa wa Roma, Papa wa sasa amepokea heshima ya kipekee katika Jumba la Kifalme la Windsor👑
Kwa idhini ya Mfalme Charles, Papa Leo XIV amekuwa Papal Confrater (Mwanachama wa Kiheshima wa Kiroho) wa Chuo cha Mtakatifu George katika Kapela ya Mtakatifu George (St George’s Chapel), Windsor, ikiwa ni ishara ya undugu wa Kikristo na urafiki.
Ni mwaka mmoja umepita tangu ilipofanyika ziara ya kihistoria ya Mfalme na Malkia huko Vatican, ambapo Mfalme Charles alikaribishwa kama Royal Confrater wa Basillika Kuu ya Mtakatifu Paulo Nje ya Kuta (St Paul’s Outside the Walls) jijini Roma.
Wafalme wa Uingereza walikuwa na uhusiano wa kihistoria na Basillika hiyo kabla ya Matengenezo ya Kikanisa (Reformation) kukata kiungo hicho. Heshima hizi za kidini za pande zote mbili ni za kwanza za aina yake katika kipindi cha nusu milenia.
Nia ya aliyekuwa Mfalme wa Uingereza (Henry VIII) ya kuvunja ndoa yake na Catherine wa Aragon, ingawa Papa alikataa kuibatilisha, ilichangia Uingereza kujitenga na Roma katika miaka ya 1530. Baadaye Bunge lilimtambua kama Mkuu wa Kanisa la Uingereza (Church of England).
Kiti kilichotengenezwa maalum kwa ajili ya Charles tayari kipo kando ya viti vya watawa jijini Roma. Na kiti kinachofanana na hicho kwa ajili ya Papa, kitazinduliwa na kuwekwa pia huko Windsor.
Baadaye, Mfalme Charles wa Uingereza atahudhuria ibada ya kuweka wakfu picha ya mozaiki ya Kristo, iliyotolewa kama zawadi binafsi na Papa Leo, katika Kikanisa cha Mtakatifu George.
Nini Hasa Kimetokea na Kwa Nini ni cha Kihistoria?
Ili kuelewa uzito wa tukio hili kati ya Mfalme Charles III na Papa Leo XIV, inabidi tuangalie muktadha wa kihistoria na hatua za sasa:
1. Chanzo cha Uhasama (Karne ya 16 / Miaka ya 1530)
Mfalme Henry VIII alitaka kuvunja ndoa yake na mke wake Catherine wa Aragon kwa sababu hakumpatia mtoto wa kiume wa kurithi kiti. Papa Clement VIII alikataa kubatilisha ndoa hiyo.
Kwa ghadhabu, Henry VIII alijitenga na Mamlaka ya Papa, na akaitangaza Uingereza kuwa huru kidini, na kuanzisha Kanisa la Uingereza (Church of England (Anglican Church) ambapo mfalme mwenyewe ndiye anakuwa Mkuu wa Kanisa. Hii ilisababisha miaka mia kadhaa ya uadui, Vita vya Kidini, na ubaguzi dhidi ya Wakatoliki nchini Uingereza.
2. Itasaidia kuupoza uhasama na kuleta undugu wa Kidini.
Heshima ya Pande Zote mbili (Reciprocal Honours): Roma kumhedhimisha Charles: Mwaka mmoja uliopita, Mfalme Charles alitembelea Vatican na akapewa cheo cha Royal Confrater huko Roma katika Basillika ya Mtakatifu Paulo. Wafalme wa kale wa Uingereza walikuwa na uhusiano na eneo hili kabla ya Henry VIII kukata mawasiliano.
Windsor kumheshimisha Papa: Sasa, Mfalme Charles amempa Papa Leo XIV cheo cha Papal Confrater katika Kapela ya Mtakatifu George iliyopo Jumba la Kifalme la Windsor.
Viti Maalum
Kama ishara ya kudumu ya udugu huu, kuna kiti maalum kilichotengenezwa kwa ajili ya Mfalme Charles jijini Roma, na kiti kingine maalum kinachowekwa Windsor kwa ajili ya Papa.
Papa amemzawadia Mfalme picha ya sanaa ya mozaiki ya Yesu Kristo, ambayo itawekwa wakfu rasmi katika ibada maalum huko Windsor.
Mfalme Charles amejulikana kwa muda mrefu kama mtu anayependa kuunganisha imani mbalimbali (Interfaith Dialogue). Hatua hii haivunji misingi ya Kanisa la Uingereza, bali inajenga daraja la amani na udugu wa Kikristo baada ya miaka 500 ya kutoelewana.
Ni hatua inayotazamwa kama moja ya mafanikio makubwa zaidi ya kidiplomasia na kiroho katika utawala wake.
“Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendeza ndugu wakae pamoja kwa umoja!” (Zab 133:1)
KRISTO SHARTI ATAWALE!
Kwa njia yake, na pamoja Naye na ndani yake; Wewe Mungu Baba Mwenyezi, katika umoja wa Roho Mtakatifu, unapata heshima yote na utukufu, milele na milele, AMINA🙏
ROZARI TAKATIFU MATENDO YA UTUKUFU (Jumatano na Jumapili)
1. Yesu anafufuka. Tumwombe Mungu atujalie kugeuka watakatifu.
2. Yesu anapaa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kwenda mbinguni.
3. Roho Mtakatifu anawashukia Mitume. Tumwombe Mungu atujalie bidii katika dini yetu.
4. Bikira Maria anapalizwa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kufa vizuri.
5. Bikira Maria anawekwa Malkia mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kudumu katika njia njema
SALA YA ASUBUHI
+Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
Tuusifu Utatu Mtakatifu wa Mungu mmoja, sasa na siku zote na milele amina. Ee utatu Mtakatifu wa Mwenyezi Mungu; +Baba, +Mwana na +Roho Mtakatifu. Ninasadiki kuwa upo hapa na mahali pote.
Ee Mungu wangu, umeniumba, umenikomboa, umenifanya mkristu, umenizidishia neema zako, umenitayarishia makao yangu mbinguni.
Ee Mungu wangu, nakuabudu, nakushukuru, nakuomba toba, nakupenda. Ee Mungu wangu, ninakutolea roho yangu, na mawazo, na maneno, na kazi na furaha, na mateso yangu, uyapokee unipe neema yako nisitende leo dhambi, Amina.
BABA YETU.
Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
Utupe leo mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni. Amina.
SALAMU MARIA.
Salamu, Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe, umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu, mzao wa tumbo lako, amebarikiwa.
Maria mtakatifu, Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
KANUNI YA IMANI.
Nasadiki kwa Mungu, Baba Mwenyezi, Muumba wa mbingu na dunia; na kwa Yesu Kristo Mwanae pekee, Bwana wetu, aliyetungwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria, akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato, akasulubiwa, akafa, akazikwa, akashukia kuzimu; siku ya tatu akafufuka kutoka wafu, akapaa mbinguni; ameketi kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi; kutoka huko atakuja kuwahukumu walio hai na wafu.
Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Kanisa takatifu Katoliki, ushirika wa Watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili, na uzima wa milele. Amina.
AMRI ZA MUNGU.
1. Ndimi Bwana Mungu wako, usiabudu miungu wengine.
2. Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako.
3. Shika kitakatifu siku ya Mungu.
4. Waheshimu baba na mama; upate miaka mingi na heri duniani.
5. Usiue.
6. Usizini.
7. Usiibe.
8. Usiseme uongo.
9. Usitamani mwanamke asiye mke wako.
10. Usitamani mali ya mtu mwingine.
AMRI ZA KANISA.
1. Hudhuria Misa takatifu Dominika na Sikukuu zilizoamriwa.
2. Funga siku ya Jumatano ya Majivu; usile nyama siku ya Ijumaa Kuu.
3. Ungama dhambi zako walau mara moja kila mwaka.
4. Pokea Ekaristi Takatifu hasa wakati wa Pasaka.
5. Saidia Kanisa katoliki kwa zaka.
6. Shika sheria katoliki za ndoa.
Ee Maria Bikira Mtakatifu, Mama wa Mungu na Mama yangu, nawe Mtakatifu Yosefu, Nawe Malaika Mlinzi wangi, Nanyi watakatifu somo wangu, nanyi Watakatifu wote, Niombeeni nipate kuacha dhambi, nilindeni siku ya leo na siku zote, na saa ya kufa kwangu, Amina.
MALAIKA WA BWANA
•Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria, Naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
~Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria mtakatifu Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
•Ndimi mtumishi wa Bwana, Nitendewe ulivyonena.
~Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria mtakatifu Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
•Neno wa Mungu akatwaa mwili, akakaa kwetu.
~Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria mtakatifu Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
Utuombee Mzazi mtakatifu wa Mungu, tujaliwe ahadi za Kristo.
Tuombe:
Tunakuomba, ee Bwana, utie neema yako mioyoni mwetu, ili sisi tuliojua kwa maelezo ya Malaika kwamba Mwanao amejifanya mtu, kwa mateso na msalaba wake utufikishe kwenye utukufu wa ufufuko. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu Amina.
SALA KWA MALAIKA MLINZI
Malaika mlinzi wangu, unilinde katika hatari zote za roho na za mwili. Amina.
Moyo Mtakatifu wa Yesu, Utuombee
Roho za waamini marehemu wapate rehema kwa Mungu wapumzike kwa amani.
+Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
Tujiandae kwa Ibada ya kesho.
Oktoba 25, 2026, DOMINIKA YA 30 YA MWAKA 'A'.
SOMO 1: Kut 22:20-26.
WIMBO WA KATIKATI
Zab 17:2-4, 47, 51.
SOMO 2: 1Thes 1:5-10.
INJILI: Mt 22:34-40.
Maandalizi mema & Dominika njema🙏