Ally Salum Hapi (@AllyHapi) header
Ally Salum Hapi (@AllyHapi) profile picture

Farmer 🇹🇿

Dar es Salaam, Tanzania
Joined March 2013
Photo by Ally Salum Hapi (@AllyHapi)Photo by Ally Salum Hapi (@AllyHapi)Photo by Ally Salum Hapi (@AllyHapi)Photo by Ally Salum Hapi (@AllyHapi)Photo by Ally Salum Hapi (@AllyHapi)Photo by Ally Salum Hapi (@AllyHapi)Photo by Ally Salum Hapi (@AllyHapi)Photo by Ally Salum Hapi (@AllyHapi)Photo by Ally Salum Hapi (@AllyHapi)Photo by Ally Salum Hapi (@AllyHapi)
Ally Salum Hapi retweeted
Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mama yetu, Mama Fatma Karume, mjane wa Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kilichotokeo leo tarehe 21 Septemba, 2026. Kifo chake ni pengo kwa familia na Taifa kwa ujumla, kwani alikuwa sehemu muhimu ya historia adhimu ya Zanzibar kuanzia wakati wa harakati za kupigania uhuru, Mapinduzi Matufuku ya Zanzibar na kuasisiwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Daima tutaendelea kukumbuka, kuenzi na kuheshimu mchango wake katika kuhifadhi kumbukumbu na urithi wetu, pamoja na kuchochea maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ya Taifa letu. Ninatoa pole kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mheshimiwa Amani Abeid Karume, familia ya Hayati Sheikh Karume, ndugu, jamaa, marafiki, wananchi wa Zanzibar na Watanzania wote. Ninawaombea Mwenyezi Mungu awajalie subra, faraja na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu. Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un.
65
107
8
353
38,363
Ally Salum Hapi retweeted
Ninawatakia Waislamu na Watanzania wote kheri na baraka za Sikukuu ya Maulid. Kumbukizi ya siku hii njema ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) itukumbushe kuendelea kuishi kwa upendo, huruma, uvumilivu na kuwajali wengine. Tusherehekee kwa amani na furaha, huku tukidumisha umoja na mshikamano wetu. Mwenyezi Mungu Mtukufu aendelee kuibariki nchi yetu, kuitunza katika amani na utulivu, na kutuwezesha kuijenga kwa maendeleo na ustawi wa wote. Mawlid Al Nabi Mubarak.
81
111
6
475
64,719
Ally Salum Hapi retweeted
Leo asubuhi nimepata heshima ya kuambatana na Mama yetu, Mama Maria Nyerere, kuelekea nchini Angola ambako pamoja na shughuli nyingine, tutashiriki uzinduzi wa Hospitali ya Rufaa iliyopewa jina la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Hii ni heshima kubwa kwa familia ya Mwalimu Nyerere na Taifa letu kwa ujumla, ikiwa ni ishara ya kutambua na kuthamini mchango wake wa kihistoria katika harakati za ukombozi na maendeleo ya Afrika.
43
103
3
391
80,725
Ally Salum Hapi retweeted
Julai 25 kila mwaka ni Siku ya Mashujaa; siku adhimu ya kuwakumbuka na kuwaenzi wote waliotoa maisha yao kupigania uhuru na kulinda amani ya nchi yetu. Kwa ujasiri, uzalendo na kujitolea kwao, walituachia msingi imara wa uhuru, amani, umoja na mshikamano tunaouenzi hadi leo. Tunapowakumbuka mashujaa wetu, tuendelee kulinda tunu walizotuachia kwa kudumisha amani, umoja na kufanya kazi kwa bidii katika kujenga Tanzania yenye maendeleo na ustawi, kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. Mungu Ibariki Tanzania.
65
83
30
211
25,181
Ally Salum Hapi retweeted
Leo nimeungana na viongozi wengine wa Afrika katika Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Afya nchini Ghana. Kupitia jukwaa hilo, nimehimiza nchi za Afrika kuongeza uwekezaji wa ndani katika sekta ya afya ili kufikia malengo ya upatikanaji wa huduma za afya kwa wote, kutokomeza UKIMWI, kuboresha huduma za afya ya uzazi na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza. Nimeeleza hatua ambazo Tanzania imechukua kuimarisha sekta ya afya, ikiwemo kuwekeza katika viwanda vya dawa na vifaa tiba, kuongeza bajeti ya afya kila mwaka, kutekeleza programu Bima ya Afya kwa Wote na kuboresha miundombinu ya huduma za afya. Maboresho hayo yanawahakikishia wananchi huduma bora za afya wakati wowote, mahali popote. Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi nyingine na jumuiya za kikanda na kimataifa kuimarisha sekta ya afya na kutafuta suluhisho la pamoja kwa changamoto za afya zinazotukabili.
24
78
2
206
30,045
Ally Salum Hapi retweeted
Shining bright ✨ #FIFAWorldCup
615
9,748
289
73,335
660,703
SPAIN WINS!
248
3,797
57
28,779
221,248
Ally Salum Hapi retweeted
4
19
47
3,427
Ally Salum Hapi retweeted
Kwa miaka 62 sasa, Tanzania na Misri zimejenga uhusiano wa kihistoria na ushirikiano imara. Ziara ya Kitaifa ya Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Mheshimiwa Abdel Fattah El-Sisi nchini Tanzania leo ni kielelezo cha uhusiano huo na dhamira yetu ya kuuimarisha kwa maendeleo ya watu wetu, kama walivyokusudia waasisi wetu. Misri ni miongoni mwa wawekezaji wakubwa nchini Tanzania. Leo tumekubaliana kuimarisha zaidi ushirikiano katika sekta za kimkakati, zikiwemo biashara na uwekezaji, kilimo, uchukuzi, afya, elimu na nishati. Kwa kuanzia, nchi zetu zimesaini hati mbili za makubaliano ya ushirikiano na tutazindua Jukwaa la Biashara ili kuchochea fursa na ustawi wa pamoja. Nimewaelekeza mawaziri na wataalamu wetu kuhakikisha makubaliano yote tuliyofikia yanatekelezwa kwa ukamilifu na kwa wakati. Wananchi wanataka kuona tija ya makubaliano haya kwenye maisha yao.
30
71
1
197
14,627
Ally Salum Hapi retweeted
Ninaipongeza Klabu ya Yanga kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa mara ya tano mfululizo. Mafanikio haya ni ushahidi wa juhudi, nidhamu na kujituma kwa wachezaji, benchi la ufundi, uongozi pamoja na mashabiki. Aidha, ninazipongeza klabu zote zilizoshiriki Ligi Kuu msimu huu kwa ushindani mzuri uliofanya mchezo wa mpira wa miguu nchini Tanzania kuendelea kukua, kuvutia na kuongeza hamasa kwa mashabiki pamoja na wadau wa mchezo huu.
70
123
10
726
31,733
Ally Salum Hapi retweeted
Ninawatakia Watanzania wote heri ya Maadhimisho ya Miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Muungano wetu ni lulu na urithi wa kipekee tulioupokea kutoka kwa waasisi wetu. Hivyo, nasi tuna wajibu wa kuutunza, kuulinda, na kuuimarisha ili tuurithishe kwa vizazi vijavyo ukiwa salama na imara kama tulivyoupokea. Ninatoa wito kwa Watanzania kuendelea kushirikiana, kufanya kazi kwa bidii, na kuimarisha uzalendo wetu, ili tujenge Tanzania moja, imara zaidi, yenye umoja na maendeleo jumuishi kwa kizazi cha sasa na kijacho. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ubariki Muungano wetu.
81
109
8
330
20,427
Ally Salum Hapi retweeted
Novemba 14, 2025 nikifungua Bunge la 13 niliahidi tutaimarisha uvuvi wa Bahari Kuu na kukuza uchumi wa buluu. Leo ninafuraha kuwa tumetekeleza hilo kwa kupata meli ya kwanza ya uvuvi wa Bahari Kuu ambayo nimeizindua mkoani Dar es Salaam. Meli hii itaongeza uzalishaji wa samaki wa Bahari Kuu, itatoa ajira, itakuza sekta ya uvuvi na mchango wake katika Pato la Taifa (GDP). Uwepo wa meli hii utatuwezesha kunufaika na uvuvi wa Bahari Kuu ambao kwa miaka mingi umefanywa na meli na kampuni kutoka nje ya nchi. Kwa kutambua kuwa takribani wananchi milioni 6 wanategemea sekta hii, tumeboresha mazingira ya uvuvi kwenye maziwa kwa kuwezesha upatikanaji wa mitaji, utaalamu, vifaa na miundombinu. Aidha, tumejipanga kujenga bandari ya uvuvi Bagamoyo, baada ya ile ya Kilwa, kununua meli nne za uvuvi na moja ya mafunzo na boti za doria. Ili tufanikishe malengo yetu nimesisitiza: 1. Tuendelee kudumisha amani na usalama 2. ⁠Nimeielekeza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kutunza mitambo tunayoinunua, na iwawezeshe wavuvi wadogo kwa masoko, vifaa, mitaji na elimu ya ujasiriamali na utunzaji fedha. Pia idhibiti uvuvi haramu na iimarishe ushiriki wa sekta binafsi kwenye uvuvi.
33
96
3
221
15,043
Ally Salum Hapi retweeted
Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Askofu wa Jimbo Katoliki Kondoa, Askofu Bernadin Francis Mfumbusa kilichotokea Aprili 14, 2026 jijini Dodoma. Pamoja na kuwatumikia wananchi kiroho, tutamkumbuka kwa umahiri wake uliochangia kukua kwa sekta ya mawasiliano nchini kupitia mafunzo na ulezi kwa wanahabari, uongozi na utafiti. Ninatoa pole kwa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Askofu Wolfgang Pisa, Maaskofu, Mapadri, Watawa, familia, ndugu, jamaa, marafiki, waumini wa Kanisa Katoliki na Watanzania wote kwa msiba huu. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina.
46
58
3
227
23,582
Ally Salum Hapi retweeted
Mapema leo katika Dua Maalum ya Kumwombea Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Mwasisi wa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, na mmoja wa waasisi wa Taifa letu. Leo ikiwa ni kumbukizi ya miaka 54 tangu kifo chake, tunamuenzi kwa ushiriki wake katika kazi kubwa ya kuweka msingi wa ujenzi wa jamii bora yenye amani, umoja, ustawi na maendeleo yanayogusa maisha ya wananchi wote.
33
68
2
190
17,881
Ally Salum Hapi retweeted
Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali ya moto ulioteketeza Soko la Mawasiliano (Simu 2000) lililopo katika Kata ya Sinza, Wilaya ya Ubungo, mkoani Dar es Salaam, jana Aprili 4, 2026. Ninatoa pole kwa wafanyabiashara waliopoteza mali zao na wananchi wote walioathirika na ajali hiyo kwa namna mbalimbali. Nimeziagiza mamlaka za uchunguzi kufanya kazi ya kubaini chanzo cha moto huo, kufanya tathmini ya madhara na hasara iliyotokea na kuchukua hatua stahiki haraka.
57
58
3
227
38,231
Ally Salum Hapi retweeted
The shooting down of two American warplanes was the most serious example of Tehran’s ability to raise the cost of the war for Washington on.wsj.com/4dsk5vp
214
1,197
52
4,397
306,441
Ally Salum Hapi retweeted
Leo ni siku ya kipekee katika sekta ya kilimo na uchumi wa nchi yetu kwa ujumla, ambapo nimezindua Benki ya Ushirika Tanzania. Benki hii ni sehemu ya kazi kubwa tunayoendelea kuifanya ya kuongeza tija katika sekta ya kilimo. Uanzishaji wa benki hii unalenga kutimiza hitaji la wananchi la upatikanaji wa mitaji kwa wakulima, hasa wakulima wadogo walioko vijijini. Hatua hii ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (2020-2025) ambapo itachochea zaidi maendeleo nchini ikiwemo ajira kwenye kilimo, ukuaji wa Pato la Taifa, upatikanaji wa malighafi za viwandani na kuhakikisha usalama wa chakula. Nimeielekeza benki hii kuwa bunifu katika kutanua wigo wa huduma zake pamoja na kusimamia kikamilifu fedha zinazotolewa, ili kujihakikishia uimara, uwezo wa kujiendesha kibiashara na uendelevu wa benki yenyewe.
153
236
7
705
56,499
Ally Salum Hapi retweeted
Kwa unyenyekevu na shukrani, nimepokea ujumbe wa hayati Papa Francisko kwangu, kwa nchi yetu na kwa Watanzania wote, aliouandika siku chache kabla Mwenyezi Mungu hajamwita kwake, na kumkabidhi Balozi wa Vatican hapa nchini, Askofu Mkuu Angelo Accattino. Tuendelee kumwombea kwa Mwenyezi Mungu alale mahali pema.
272
244
23
899
110,511
Ally Salum Hapi retweeted
Nawashukuru nyote kwa salamu nyingi za kheri na upendo katika kumbukizi ya miaka minne ya Kiapo cha kuitumikia nchi yetu katika nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tuungane pamoja kumuomba Mwenyezi Mungu aendelee kuibariki nchi yetu, tudumu katika umoja, amani na utulivu. Tumuombe pia Mwenyezi Mungu aendelee kutuongoza katika utu na weledi kwenye utekelezaji wa majukumu yetu, na kuzibariki kazi tunazozifanya katika kuleta ustawi wa nchi yetu na Wananchi wote. Kazi na Utu, Tunasonga Mbele.
430
385
32
1,391
79,991
Ally Salum Hapi retweeted
Korosho 📌📌📌📌📌📌
17
27
2
85
9,911