Pinned Tweet
Follow the Fahamu kwa Haraka channel on WhatsApp:
Crypto | Blockchain | Finance | Economics
Elimu na uchambuzi kwa Waswahili.
Mwelekeo wa maarifa, siyo ushauri wa kifedha.
DYOR | NFA whatsapp.com/channel/0029VaJ…
1
3
602
🇹🇿Fahamu kwa Haraka retweeted
Kuna kitu kimoja kinaniumiza sana kuhusu Twitter kufungiwa Tanzania.
Na nataka kuwaambia kwa nini.
Mimi binafsi, Twitter imebadilisha maisha yangu.
Vitu vingi nilivyojifunza kuhusu teknolojia, startups, AI na kujenga biashara, nimejifunza kupitia Twitter.
Na sio kujifunza tu.
Kupitia Twitter nimepata wawekezaji kutoka Marekani ambao wamewekeza kwenye kampuni yetu ya NALA.
Nimekutana na watu ambao nimewaajiri. Nimejenga urafiki na mahusiano na watu ambao leo tunafanya nao kazi NALA.
Watu ambao pengine nisingekutana nao maishani mwangu!
Na mpaka leo, natumia Twitter kujifunza kila siku.
Hasa sasa hivi, natumia Grok bot, AI ya Twitter, zaidi na zaidi. Naendelea kujifunza, kuuliza maswali, na ku-connect na watu wenye maarifa kutoka duniani kote.
Sasa fikiria kijana wa miaka 20 aliyepo Mwanza, Mbeya au Kigoma.
Ana simu. Ana internet. Hana connection za Silicon Valley. Hana pesa ya kwenda vyuo vikubwa duniani.
Lakini kupitia Twitter anaweza kujifunza, kukutana na investors, kupata kazi, au hata kupata mtu wa kujenga naye kampuni.
Hiyo ndiyo nguvu ya Twitter!
Na ndiyo maana nimesikitishwa sana kwamba Twitter imefungiwa Tanzania.
Kwa sababu kwangu, Twitter haikuwa tu social media.
Ilikuwa darasa langu. Ilikuwa sehemu ya kujenga biashara. Ilikuwa sehemu ya kupata marafiki na connections duniani.
Na naamini kuna vijana wengi wa Tanzania ambao wanaweza kupata fursa kama nilizopata mimi.
Swali langu kwenu ni hili: Twitter imewahi kukufungulia mlango gani kwenye maisha yako?
*Somo la 26: Kwa Nini Bitcoin Wallets Zinahitajika?*
What is the purpose of using a Bitcoin wallet?
Kwa nini tunahitaji kutumia Bitcoin wallet?
Kwa nini crypto wallet inahitajika?
Ili kuelewa kwa nini Bitcoin wallets zinahitajika, kwanza tunahitaji kuangalia mfumo wa kawaida wa kuhamisha pesa kati ya watu wawili kwa kutumia.... akaunti za benki.
Mfumo wa kawaida wa benki
Ili kufuatilia pesa za kila mteja, benki huweka ledger inayorekodi salio la kila akaunti kulingana na namba ya akaunti.
Hii ni mfano rahisi:
Account| Balance
001| TZS 10,000
002| TZS 20,000
003| TZS 50,000
Ledger hii inasimamiwa na administrator.
Ni administrator huyu anayewapangia wateja namba za akaunti, na mteja anapotaka kufanya malipo, anatuma ombi kwa administrator.
Ili administrator aweze kutekeleza ombi hilo, lazima kuwe na aina fulani ya authentication, ambapo mteja anathibitisha kwamba yeye ndiye mmiliki halisi wa akaunti.
Kwa hiyo, benki inaweza kutengeneza username na password inayohusishwa na kila akaunti.
Kama unajua username na password iliyowekwa kwenye akaunti fulani, hii inatumika kuthibitisha kwamba wewe ndiye mmiliki wa akaunti hiyo.
Account| Username| Password| Balance
001| Joeli| 9876| TZS 10,000
002| Anna| 1234| TZS 20,000
003| Bizo| 5511| TZS 50,000
Administrator ndiye anayetoa au kukataa access kwenye akaunti, na pia ndiye anayesimamia kuhakikisha salio la kila akaunti ni sahihi.
Administrator anahakikisha kwamba hakuna mtu anayetumia pesa ambazo hana kwenye akaunti yake, au kutumia pesa zilezile zaidi ya mara moja (double spending).
Tatizo kwenye digital currency iliyodecentralize
Kwa digital currency iliyodecentralize kama Bitcoin, hii inaleta tatizo.
Kutegemea administrator kunaleta tatizo la centralization.
Huwezi kuwa katika control kamili ya akaunti yako!
Administrator ndiye mwenye control.
Administrator anaweza:
- Kukunyima access kwenye akaunti yako.
- Kuzuia au kuchuja (censor) transactions.
- Kukataa kukuruhusu kufungua akaunti kabisa.
Kwa mfano, benki zina mamlaka ya kufunga akaunti zako.
Pia zinaweza kureverse transactions na kufreeze accounts.
Fikiria umeenda kula dinner na mtu unayempenda sana, halafu muda wa kulipa bill unafika, unagundua kwamba benki yako imekataa transaction kwa sababu tu imeamua kutofanya biashara na hiyo restaurant.
Hilo lingekuwa jambo la aibu sana. 😅
Mtu uliyeenda naye anaweza kudhani huna pesa kabisa. 🤦
Kila unapokuwa na entity yenye uwezo wa ku-approve au ku-deny kitu fulani, unakuwa chini ya control ya third party ya kati (centralized third party).
Bitcoin inatatua tatizo hili vipi?
Ili decentralized digital currency iweze kufanya kazi, mtu yeyote anapaswa kuwa na uwezo wa kufungua “account” na kufanya transactions na mtu yeyote anayemtaka.
Hupaswi kuomba permission.
Kwa hiyo, solution ni ipi?
Ondoa administrator.
Lakini je, inawezekana kutengeneza “account” bila administrator?
Ndiyo. 👍
Bitcoin ina solution:
Badala ya kutumia account numbers, Bitcoin inatumia addresses.
_Bitcoin Address_ | *BTC*
_1DmjiSdcaSUPyqEuhqHkLrudpJUYDXct5s_ | *2*
_3QqQAx4ToxsiiFtXbrDkuCSBGYKd56vTzU_ | *15*
_1PhGCKEeLjCo6ZGz9NAKL3FvCZACLbV1DC_ | *3*
Unapataje Bitcoin address?
Unachohitaji ni wallet.
Kuna wallets nyingi ambazo unaweza ku-download bure kutoka kwenye internet.
Kwa kutumia addresses badala ya account numbers, mtu yeyote anaweza kutengeneza “account” yake mwenyewe kupitia wallet software kwenye computer au simu yake, bila kuomba administrator ampe account number.
Unaweza kutengeneza addresses nyingi kadri unavyotaka, na wallet software yako itazisimamia zote kwa ajili yako.
Kwa hiyo, tofauti na bank account, address inaweza kutengenezwa na mtu yeyote ndani ya muda mfupi, bila kuhitaji third-party administrator.
Bitcoin ni Permissionless
Matumizi ya addresses, ambazo wallet inakutengenezea bure, yanaifanya Bitcoin kuwa permissionless.
1
331
Permissionless maana yake ni kwamba mtumiaji wa Bitcoin hahitaji kupata permission kutoka kwa mtu au taasisi fulani ili kujiunga na Bitcoin network.
Wallets zinampa mtu wa kawaida uwezo wa kufanya permissionless transactions bila kuhusisha third parties na bila kuhitaji kujisajili na taasisi fulani.
Wallets pia zinafanya Bitcoin na crypto nyingine ziweze kufikiwa na watu wengi zaidi.
Kama una internet connection, unaweza:
1. Ku-download wallet app.
2. Kui-install.
3. Kutengeneza Bitcoin address.
4. Na tayari unaweza kuanza kutumia Bitcoin.
Hatuhitaji permission kutumia Bitcoin
Hatuhitaji permission ya mtu ili kutumia Bitcoin au cryptocurrency nyingine!
Crypto inaweza kusaidia kuongeza financial inclusion, kwa kutoa access rahisi kwa bidhaa na huduma za kifedha kama payments kwa watu ambao hawana kabisa huduma za benki au ambao huduma hizo ni chache.
Kama unasoma somo hili, unaweza kuanza kutumia Bitcoin.
Mtu yeyote duniani anaweza kushiriki, mradi tu awe na kifaa kinachoweza ku-connect kwenye internet.
Huhitaji kuomba kufungua account kwenye benki au corporation nyingine ili uweze kutuma na kupokea bitcoins.
Hii ndiyo purpose ya Bitcoin wallets, na ndiyo sababu wallets ni muhimu sana.
97
Ili uweze kutuma au kupokea Bitcoin, unahitaji kutumia “Bitcoin Wallet” (pochi ya Bitcoin).
Katika masomo yanayokuja utajifunza:
Bitcoin Wallet ni nini
Aina mbalimbali za Bitcoin Wallet
Jinsi kila aina inavyofanya kazi
Jinsi ya kutumia Bitcoin Wallet kutuma na kupokea Bitcoin
Let's Gooo👇😀
whatsapp.com/channel/0029VaJ…
236
*Somo la 23: Ni Nini Kinachofanya Blockchain Kuwa ya Kipekee?*
Blockchain hiki. Blockchain kile.
Katika somo lililopita, nilikupa maelezo ya msingi ya kiufundi kuhusu blockchain. Natumaini hayakuwa ya kuchosha sana.
Sasa kwa kuwa unajua blockchain ni nini...
Ni nini kinachoifanya teknolojia ya blockchain kuwa ya kipekee sana?
Kuuliza "Blockchain ina nini cha pekee?" ni sawa na kuuliza:
Internet ina nini cha pekee?
Umeme una nini cha pekee?
Balbu ya taa ina nini cha pekee?
Au hata kuuliza kwa nini chipsi za McDonald's zinazotoka moja kwa moja kwenye mafuta huwa tamu sana.
Ndiyo, blockchain ni teknolojia muhimu kiasi hicho.
Hebu tuone kwa nini.
*Kabla ya Blockchain*
Kabla ya blockchain, kama ulikuwa na taarifa muhimu sana unazotaka kuhifadhi kwenye kompyuta, ulihitaji mtu au taasisi fulani kumiliki na kudhibiti taarifa hizo.
Hii ilimaanisha lazima kuwe na mamlaka ya kati (Central Authority).
Kwa mfano, salio la akaunti yako benki.
Benki ndiyo inayomiliki taarifa hizo na ndiyo yenye mamlaka ya kubadilisha salio lako.
Benki huhakikisha kwamba kila muamala ni halali na umeidhinishwa na mwenye akaunti.
Huwezi kwenda moja kwa moja kwenye mfumo wa benki ukabadilisha salio lako, hata ukiomba kwa heshima.
Kwa hiyo benki hulazimika kuajiri wataalamu wa usalama wa mifumo (IT Security) ili kulinda taarifa hizo dhidi ya wahalifu wa mtandao (hackers) na watu wasioidhinishwa.
Hata Kabla ya Kompyuta
Tatizo hili lilikuwepo hata kabla ya kompyuta.
Ili kuhifadhi kumbukumbu za fedha au miamala, ilibidi kuwe na mtu mmoja au taasisi moja inayohusika kuzisimamia.
Huyu ndiye alikuwa Central Authority.
Kazi yake ilikuwa kuhifadhi kile kinachoitwa Ledger.
Ledger ni kitabu kinachorekodi historia ya miamala.
Zamani ledger ilikuwa ni:
Karatasi
Au daftari lililotengenezwa kwa ngozi
Ambalo lilikuwa linaandikwa kwa mkono na kuhifadhiwa sehemu salama, kama kwenye droo ya ofisini.
Baada ya Kompyuta Kuvumbuliwa
Kompyuta zilipoanza kutumika, ledger ikahamishiwa kwenye database iliyohifadhiwa ndani ya hard drive ya kompyuta moja.
Baadaye watu wa IT wakagundua kuwa si salama kuweka database kwenye kompyuta moja tu.
Kwa nini?
Kwa sababu:
Hard drive inaweza kuharibika.
Kompyuta inaweza kuungua.
Inaweza kuibiwa.
Data yote ingeweza kupotea.
Ndiyo maana database ilianza kunakiliwa (replicated) kwenye kompyuta nyingine kadhaa.
Lakini...
Hata kama kulikuwa na nakala nyingi, bado kulikuwa na database moja kuu (Official Database).
Na database hiyo bado ilisimamiwa na mamlaka ya kati.
Tatizo la Mfumo wa Central Authority
Kwa kuwa kulikuwa na sehemu moja kuu ya kuhifadhi taarifa...
Mtu akifanikiwa kuingia kwenye database hiyo...
Anaweza kubadilisha taarifa.
Kwa mfano, kuongeza sifuri kadhaa kwenye salio lake la benki.
Mfumo huu wa kutegemea sehemu moja ndiyo ulikuwa udhaifu mkubwa.
Je, Kulikuwa na Njia Bora Zaidi?
Je, ingewezekana kuwa na ledger ambayo:
Haina benki inayoidhibiti?
Haina serikali inayoisimamia?
Haina kampuni inayomiliki?
Hapo ndipo blockchain ilipozaliwa.
Blockchain Ilileta Suluhisho
Kabla ya Satoshi Nakamoto, hakuna aliyekuwa amefanikiwa kutengeneza mfumo wa Decentralized Ledger.
Lakini Satoshi alipata suluhisho.
Badala ya kuwa na mmiliki mmoja wa database...
Aliamua kuiweka database kwenye mtandao wa kompyuta nyingi.
Blockchain Network
Mtandao huu ni mkusanyiko wa kompyuta nyingi zilizopo sehemu mbalimbali duniani ambazo zimeunganishwa kupitia Internet.
Kila kompyuta huhifadhi nakala yake binafsi ya database.
Hii ina maana hakuna database kuu.
Kwa blockchain...
Kila nakala ndiyo database rasmi.
Hakuna inayozidi nyingine.
Ndiyo maana mfumo huu unaitwa:
Distributed Ledger.
Kwa sababu ledger imesambazwa kwenye kompyuta nyingi duniani.
Blockchain ni ya Wazi (Public)
Kila mtu anaweza kuona blockchain.
Mabadiliko yote yanayoingia yanaonekana kwa wakati halisi (real time).
Hakuna anayeficha taarifa.
Blockchain Iliondoa Central Authority
1
265
Blockchain iliondoa hitaji la kuwa na taasisi moja inayomiliki data.
Badala yake...
Kompyuta zote kwenye mtandao hukubaliana pamoja kuhusu taarifa zipi ziandikwe.
Makubaliano hayo huitwa:
Consensus.
Consensus Inafanyaje Kazi?
Kompyuta zote zinafuata sheria zilezile.
Sheria hizi zimeandikwa kwenye programu inayoitwa:
Protocol.
Protocol ndiyo inayowaambia nodes:
Muamala upi ni halali.
Block ipi ikubalike.
Block ipi ikataliwe.
Kompyuta zote zinaendesha software yenye protocol hiyo hiyo.
Mfano Rahisi
Fikiria mpo kwenye kikundi.
Kuna njia mbili za kufanya maamuzi.
Njia ya kwanza
Mtu mmoja ndiye anaamua kila kitu.
Hii ndiyo Central Authority.
Njia ya pili
Kila mtu anakubaliana kwanza ndipo uamuzi ufanyike.
Hii ndiyo Consensus.
Blockchain hutumia njia ya pili.
Blockchain Ilivunja Historia
Hebu fikiria maelfu ya watu duniani:
Hawafahamiani.
Hawaaminiani.
Hawana kiongozi mmoja.
Lakini wote wanakubaliana kuwa historia ya miamala kwenye blockchain ni sahihi.
Na yote haya yanafanyika bila benki, serikali au kampuni kuthibitisha.
Hii ndiyo akili kubwa ya blockchain.
Blockchain Iliondoa Middleman
Blockchain iliondoa mtu wa kati (Middleman).
Badala ya kusema:
> "Mimi ndiye nitakayesimamia ledger."
Blockchain inasema:
> "Sisi sote tutakuwa na nakala ya ledger na tutaendelea kuihifadhi pamoja."
Decentralized Trust
Blockchain ilihamisha mamlaka ya kufanya maamuzi kutoka kwa taasisi moja kwenda kwa mtandao wa kompyuta nyingi.
Hii ndiyo inaitwa:
Decentralized System of Trust.
Mfumo wa kuaminiana ambao hautegemei taasisi yoyote.
Kwa Nini Hii Ni Mafanikio Makubwa?
Kwa mara ya kwanza duniani...
Iliwezekana kuhifadhi taarifa muhimu kwenye kompyuta nyingi ambazo haziaminiani.
Lakini taarifa zenyewe zikabaki kuwa sahihi na salama.
Hili halikuwahi kufanyika kabla.
Blockchain ni Teknolojia Muhimu Sana
Leo blockchain imewekwa kwenye kundi la teknolojia zilizobadilisha dunia, kama vile:
Steam Engine
Umeme
Kompyuta
Internet
Na hata Selfie 😄
Blockchain Sio ya Bitcoin Pekee
Ingawa Bitcoin ndiyo matumizi maarufu zaidi ya blockchain...
Leo blockchain inatumika pia kwenye cryptocurrencies nyingine nyingi.
Kwa mfano:
Ethereum
BNB Chain
Solana
Cardano
Polkadot
Avalanche
Cosmos
Na nyingine nyingi.
Hitimisho
Blockchain ni teknolojia iliyobadilisha kabisa namna taarifa zinavyohifadhiwa na kusimamiwa. Badala ya kutegemea mtu mmoja au taasisi moja, blockchain hutumia mtandao wa kompyuta nyingi zinazofuata sheria zilezile na kufikia makubaliano (consensus). Hii ndiyo sababu blockchain ni salama, ni wazi, ni ngumu sana kubadilisha taarifa zilizorekodiwa, na ndiyo msingi unaowezesha Bitcoin na cryptocurrencies nyingine kufanya kazi bila kutegemea mamlaka ya kati.
89
*Jipange na Crypto!*
_Kama Hujui Chochote Kuhusu Crypto, Usihofu cha kwanza jiunge kwenye channel yetu
whatsapp.com/channel/0029VaJ…. Kisha fuata hatua hizi
*1. Jiunge na Binance* jukwaa kubwa la kuaminika duniani.
🟡 Tumia referral code: JOINBITCOIN
🌐 accounts.binance.com/registe…
✅ Salama
✅ Rahisi kutumia
✅ Bonasi kwa wanaojiunga!
*2. Verify Akaunti (KYC)*
Tumia majina yako sahihi kama kwenye ID.
Chagua ID:
NIDA
Passport
Driving License
Voter ID (Mpiga kura)
Upload ID yako kwa njia zifuatazo:
Piga picha moja kwa moja.
Au upload ID iliyohifadhiwa kwenye simu yako.
*Muhimu:*
Scan ID pande zote mbili.
Hakikisha background ni nyeupe.
Mwanga wa kutosha bila kutumia flashlight.
Jina liendane na ID.
Facial Verification:
Usivae miwani, kofia, au vitu vinavyofunika uso.
Hakikisha mwanga ni wa kutosha.
*Kumbuka:*
Kama huna ID, tembelea ofisi ya NIDA ujisajili.
*3. Documents Zinazokubalika Tanzania kwa KYC*
Passport
Driving License
National ID (NIDA)
Voter ID (Mpiga kura)
*NOTE:*
*Fuata hatua zote kwa makini ili uanze safari yako ya crypto kwa mafanikio!*
282
*Somo la 18: Bitcoin Mining ni Nini?*
Swali ambalo watu wengi huuliza ni:
*Bitcoin Mining ni nini?*
Kwa lugha rahisi,
Bitcoin Mining ni mchakato wa kuthibitisha miamala ya Bitcoin na kuiongeza kwenye Blockchain.
Kompyuta zinazofanya kazi hii huitwa:
Bitcoin Miners (Wachimbaji wa Bitcoin).
Mbali na kuthibitisha miamala, wachimbaji pia hupokea bitcoin mpya kama zawadi kwa kazi wanayoifanya.
*Kwa Nini Bitcoin Inahitaji Mining?*
Ili kuelewa vizuri umuhimu wa mining, kwanza fikiria Bitcoin isingekuwa na mining kabisa.
*Hatua ya Kwanza*
Fikiria kuna faili moja kubwa.
Faili hilo ndilo:
Blockchain
Blockchain ni ledger iliyosambazwa (Distributed Ledger) ambayo huhifadhi miamala yote iliyothibitishwa.
Kwa sasa kumbuka tu kwamba blockchain ni kumbukumbu ya miamala yote ya Bitcoin.
*Hatua ya Pili*
Sasa fikiria kuna maelfu ya kompyuta duniani kote.
Kompyuta zote:
- Zimeunganishwa kupitia internet.
- Zinatumia programu ya Bitcoin.
- Kila moja ina nakala ya blockchain.
Hizi ndizo Bitcoin Nodes.
*Hatua ya Tatu*
Sasa unataka kumtumia mtu bitcoin.
Unaanzisha muamala (transaction).
Muamala huu ni taarifa ndogo inayoeleza:
"Namtumia mtu fulani kiasi fulani cha bitcoin."
Kama Mining Isingekuwepo
Muamala ungefika kwenye node moja.
Node hiyo ingeandika moja kwa moja muamala huo kwenye blockchain yake.
Baadaye ingeutuma kwa node nyingine.
Node hizo nazo zingeandika kwenye blockchain zao.
Hatimaye muamala ungeenea kwenye mtandao mzima.
Na kila node ingekuwa imehifadhi taarifa hiyo.
Kwa mtazamo wa kwanza, mfumo huu unaonekana kufanya kazi vizuri.
Lakini kuna tatizo kubwa sana.👇🏿
whatsapp.com/channel/0029VaJ…
Karibu *Fahamu kwa Haraka* , Mimi nitakuwa kiongozi wako katika safari hii.
Kama wewe ni mgeni kwenye cryptocurrencies, umefika sehemu sahihi. Nimetengeneza hii course ili iwe rahisi kwa beginner kuelewa soko la crypto.
Nitakupa maelezo rahisi kueleweka kuhusu Bitcoin, altcoins, tokens, na soko la crypto kwa ujumla.
Ufahamu wa crypto unaendelea kukua kila siku.
Kila siku watu wengi zaidi wanaingia kwenye crypto, wengine kwa sababu wanaamini teknolojia hii inaweza kubadilisha dunia, na wengine kwa sababu ya FOMO (hofu ya kupitwa).
Lakini pamoja na hii interest kuongezeka
pia kumekuwa na ongezeko la ushauri unaoleta wasiwasi na taarifa zisizo sahihi.
Kila siku kuna scammers wanaotafuta nafasi ya kukuingiza kwenye mtego. Twende sasa mdogo mdogo👇🏽 *See More*
1
263
*1. Elewa kuwa crypto ina risk*
Crypto ina hatari, na unatakiwa kuchukua muda kuielewa.
*2. Usikimbilie kuingia*
Watu wengi wapya wanafanya kosa moja kubwa:
Wanataka kuingia FAST ili wapate profit ya haraka na kuwa matajiri upesi.
*3. Usifanye kama kamari*
Ni kawaida kuona watu TikTok, Twitter na Reddit wanacheza na pesa zao kama kamari wakitaka kununua “lambo”.
*4. Crypto sio get-rich-quick scheme*
Kama ilivyo kwenye forex hii SIYO njia ya kutajirika haraka.
Hautasikia hapa: 👉 “Weka pesa leo, kesho utoke tajiri”
*5. Tumia conservative approach*
Weka sehemu NDOGO tu ya mtaji wako kwenye crypto.
*6. Manage risk yako vizuri*
Crypto ni speculative sana.
Kama hu-manage risk: 👉 Uwezekano wa kupoteza pesa nyingi au zote ni mkubwa.
Usijekuamini maneno kama haya:
“Usijali kama huelewi. Wanaoelewa wanasema hii kitu itakuja kuwa kitu kikubwa sana! Hii ndiyo next big thing!”
*Mimi nakataa.*
👉 _UNATAKIWA kuelewa._
Unatakiwa:
- Kufanya maamuzi kwa akili
- Kujua unanunua nini
- Kuelewa risk zake
- Kujua jinsi ya ku-manage risk
Baadaye ukiwa na wajukuu wako ungependa kuwaambia nini kati ya hivi?
1 - “Nilikosa opportunity na nilipitwa na crypto.”
2 - “Niliweka maisha yangu yote kwenye crypto na nikapoteza kila kitu kwa sababu sikuwa naelewa… nikadanganywa na matapeli… ndio maana bado ninaishi maisha haya na bibi yako.”😅
_Tunataka usiwe hata mmoja wao._
Ni muhimu sana kuwa na uelewa wa msingi wa technology na concept za crypto kabla ya kuweka hata shilingi moja.
Lengo la hii course ni kukupa msingi imara kama wewe ni beginner unaeanza safari ya crypto.
Mwisho wa hii course: 👉 Utaweza kuamua kama crypto inakufaa au la.😀
FAHAMU KWA HARAKA
75
Watu wengi wanaona crypto kama hela ya mtandaoni tu… lakini ukweli ni kwamba crypto ni aina mpya kabisa ya uwekezaji ambayo watu wengi bado hawaijaelewa vizuri.
Kwenye somo lililopita ulijifunza crypto ni nini na kwa nini ni tofauti na pesa za kawaida.
Lakini kuna kitu muhimu zaidi:
Crypto siyo tu pesa ya kutumia kununua vitu.
Ukweli ni huu:
- Watu wengi wanaitumia kama uwekezaji
- Wengine wanaitumia kufanya biashara ya kununua na kuuza (trading)
Ni sawa na mtu kununua dhahabu au kiwanja akitegemea bei ipande baadae.
Crypto ni asset kama zilivyo nyingine
Kuna aina tofauti za uwekezaji ambazo watu wamezoea:
- Hisa
- Bond
- Nyumba na ardhi
- Dhahabu na bidhaa nyingine
- Pesa/Cash
Sasa kuna kundi jipya limeongezeka: crypto
Sekta ya fedha za kawaida bado haijakubaliana kama crypto ni asset halisi au la.
Hoja kubwa ni hii:
“Crypto haina mapato wala gawio (dividends), hivyo ni ngumu kupima thamani yake.”
Lakini kumbuka:
Hata dhahabu haina gawio, lakini ina thamani kubwa
Crypto inaweza kuangaliwa kama asset, na zaidi ya hapo, ni aina mpya kabisa ya uwekezaji.
Lakini, bado ni uwekezaji wenye hatari kubwa (speculative)
Hata Jerome Powell alisema:
Watu wanatumia Bitcoin kama asset ya kubahatisha, kama dhahabu… ila ya kidigitali
*Bitcoin kama hifadhi ya thamani*
Taratiibu, Bitcoin inaanza kuonekana kama sehemu ya kuhifadhi thamani kimataifa.
Hii inaonekana zaidi kwenye nchi au mazingira ambayo watu hawaamini pesa zao za kawaida.👇 *See More*
1
274
Serikali inaweza kuchapisha pesa mpya kesho na thamani ya pesa yako ikashuka, lakini kuna aina ya pesa ambayo HAIWEZI kufanyiwa hivyo. Hii ndiyo siri ambayo mabenki hawataki uijue.
Sasa niambie, umewahi kutuma pesa kupitia M-Pesa kwenda kwa mtu wa mkoa mwingine?
Vizuri. Umetumia mtandao wa Vodacom, umelipa ada yao, na wao wamekupa ruhusa ya kutuma pesa.
Cryptocurrency inafanya kitu hicho hicho lakini bila Vodacom. Bila benki. Bila serikali. Na bila kuhitaji ruhusa ya mtu yeyote.
Hiyo ndiyo nguvu yake kubwa.👇
CRYPTOCURRENCY NI NINI HASA?
Fikiria cryptocurrency kama pesa ya kidigitali haionekani kwa macho, haigusiki, haina karatasi wala sarafu.
Inapatikana kwenye mtandao tu. Kama ujumbe unaotuma WhatsApp hauonekani, lakini unafika.
Tofauti na shilingi ya kawaida, cryptocurrency haidhibitiwi na serikali yoyote wala benki yoyote duniani.
1️⃣ NI YA KIDIGITALI
Hakuna noti wala sarafu.
Ipo kwenye mfumo wa kompyuta (code) pekee.
Ni kama picha au video kwenye simu yako huioni kwa macho moja kwa moja, lakini ipo na unaweza kuitumia.
2️⃣ HAINA MIPAKA
Fikiria hili:
Ukituma pesa kwenda Kenya kupitia benki inaweza kuchukua siku 2–3, ada ni kubwa, na benki ina mamlaka ya kuamua kama muamala ufanyike au la.
Lakini kwa cryptocurrency?
Unatuma papo hapo. Inafika ndani ya dakika chache. Popote duniani. Na ada ni ndogo sana.
Mtu wa Dar es Salaam anaweza kutuma crypto kwa mtu wa Japan sawa kabisa na kutuma txt WhatsApp.
3️⃣ HAITAJI RUHUSA
Benki inaweza kukunyima akaunti kwa sababu ya historia ya mkopo, umri, au kukosa nyaraka.
Kwa crypto hakuna hayo.
Hakuna kujaza fomu. Hakuna usaili. Hakuna kukataliwa.
Unachohitaji ni simu yenye internet na tayari unaweza kuanza kuitumia.
4️⃣ INA FARAGHA (PRIVACY)
Badala ya kutumia jina lako, unatumia “address” ambao ni mchanganyiko wa namba na herufi za kompyuta.
Ni kama sanduku la posta lisilo na jina, unaweza kupokea pesa bila watu kujua wewe ni nani.
5️⃣ HAINA MMILIKI (DECENTRALIZED)
Shilingi yetu inasimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT). Wanaweza kuongeza kiwango cha pesa wakati wowote jambo linaloweza kushusha thamani yake.
Dollar inasimamiwa na Federal Reserve ya Marekani.
Euro inasimamiwa na taasisi za Ulaya.
Lakini Bitcoin haina mmiliki.
Haidhibitiwi na nchi yoyote, benki yoyote, wala mtu yeyote.
Sheria zake zimeandikwa kwenye mfumo wa kompyuta na haziwezi kubadilishwa kiholela.
6️⃣ NI SALAMA HAIWEZI KUIGWA
Hii ni sehemu ya kisayansi kidogo, lakini rahisi kuelewa:
Neno “crypto” linatokana na “cryptography” sayansi ya kulinda taarifa kwa kutumia hesabu ngumu za kihisabati.
Fikiria kama kufuli la kisasa sana ambalo haliwezi kuvunjwa kirahisi.
Ndiyo maana cryptocurrency haiwezi kuigwa wala kudanganywa.
UKWELI AMBAO WENGI HAWAELEWI
Watu wengi wanaona crypto kama kamari au mchezo wa bahati nasibu.
Lakini ukweli ni huu:
Cryptocurrency ni teknolojia mpya ya fedha kama vile simu za mkononi zilivyobadilisha mawasiliano miaka 20 iliyopita.
Zamani watu waliuliza:
“Nani atatumia simu badala ya simu ya mezani?”
Lakini walioelewa mapema walinufaika sana.
Leo hii watu wanauliza:
“Nani atatumia crypto badala ya benki?” 🤔
Historia inajirudia swali ni wewe uko upande gani.
101
🇹🇿Fahamu kwa Haraka retweeted
Unemployment rate rising
Geopolitical conflicts rising
Price of oil rising
Inflation rising
Airport travel collapsing
Bitcoin dropping
Stocks dropping
All business cycles must come to an end, and it usually ends with a recession.
- Blockchain inaleta equality inaondoa ukoloni mambo leo.
-Blockchain inatupa uwezo wa kuwajibisha au kuishtaki Ai.
Kama AI inaweza kujifunza kazi yoyote haraka kuliko binadamu…
Je, ni ujuzi gani utabaki kuwa wa thamani kwa binadamu?
Fikiria hilo.
FAHAMU KWA HARAKA
🇹🇿Fahamu kwa Haraka retweeted
Aiseee.! Fikiria mtu amejaribu ku-swap 50M $USDT zote kwenda $AAVE zenye thamani ya $36K. Na siyo kwa bahati mbaya tu kabla hajathibitisha alipewa warning kwamba process itapelekea kupata hasara kubwa yrye hakujali akabonyeza comfirm matokeo yake ni hasara kubwa isiyo ya kawaida. Hawa ndio wale newbies mazee ya taptap anatukia tu industry bila kujua hata basics 😂





