Buddy retweeted
Tumshukuru Mungu sana kwa maisha ya Tundu Lissu. Mwaka na miezi nane iliyopita umekuwa wa kujitoa mhanga kwa ajili ya nchi yetu. What a Man!!
Buddy retweeted
“Wana Chadema wenzangu,
Kukatishwa tamaa ni jambo la kweli. Kuchoshwa na hali iliyopo ni jambo lisiloepukika. Kuvunjika moyo ni sehemu ya ubinadamu. Lakini kujisalimisha kwa watesa wetu hakupaswi kamwe kuwa hitimisho la historia yetu ya pamoja.”
Buddy retweeted
Binafsi naamini Tundu Lissu anatabasamu moyoni huku akijisemea yale maneno ya Yesu:
Msinililie mimi; jililieni ninyi na watoto wenu.
Tundu ni champion wa civil disobedience.
Kama walivyo watangulizi wake: Yesu, Mahatma Gandhi, Martin Luther, Nelson Mandela, Henry Thoreau, etc., amechagua kukataa kutii kwa sababu anaamini ndio njia sahihi ya kupambania haki.
Anajua wazi hatari iliyopo mbele yake lakini bado anafanya alivyofanya kwa sababu anaamini ndio jambo sahihi.
Wanaamini kwenye yale maneno ya Gandhi aliposema:
"They may torture my body, break my bones, even kill me. Then they will have my dead body, not my obedience."
Imani ya Tundu Lissu ni kuyaishi yale ambayo Mitch Leigh aliyeweka kwenye midomo ya Don Quixote wa Man of La Mancha:
To dream the impossible dream,
To fight the unbeatable foe,
To bear with unbearable sorrow,
To run where the brave dare not go.
To right the unrightable wrong,
To love pure and chaste from afar,
To try when your arms are too weary,
To reach the unreachable star.
This is my quest,
To follow that star --
No matter how hopeless,
No matter how far.
To fight for the right
Without question or pause,
To be willing to march into hell
For a heavenly cause.
And I know if I only be true
To this glorious quest
That my heart will lie peaceful and calm
When I'm laid to my rest.
And the world will be better for this
That one man scorned and covered with scars
Still strove with his last ounce of courage.
To fight the unbeatable foe.
To reach the unreachable star.
Kwa hiyo, badala ya sisi kulia na kumwonea huruma, tunapaswa kujiangalia ndani yetu na kutafakari namna tunavyoshiriki kuhalalisha ushenzi anaopambana nao.
Uchungu wa ukweli ni kukataa kuendelea kutumika kukawaidisha na kurudufisha hali.
Uchungu wa kweli ni kuhakikisha mbegu aliyoipanda Lissu inamea na kuzaa matunda.
Kwa maneno yale yale ya Yesu: ANAKUFA ILI WENGI WAPATE KUPONA.
Tutafika.
Buddy retweeted
SIMAMA, UHESABIWE — USIWE KATIKATI!
Rev Peter Simon Msigwa
Kwa wanasiasa na wanaharakati wa Tanzania.
Mambo ni mawili, wala si matatu!
Ama usimame upande wa watekaji, wauaji na wakandamizaji,
Au usimame upande wa haki, uhuru, demokrasia na maendeleo.
USIWE KATIKATI!
Maana kuna nyakati ukimya ni sauti,
Kuna nyakati kutokuchagua ni kuchagua,
Na kuna nyakati kusimama katikati ni kusimama upande wa mwenye nguvu dhidi ya asiye na nguvu.
SIMAMA, UHESABIWE!
Usisubiri upepo ubadilike ndipo utandike tanga.
Usisubiri jua lichomoze ndipo ukiri kuwa usiku ulikuwa na giza.
Usisubiri minyororo ikatike ndipo ujitangaze kuwa ulipenda uhuru.
Usisubiri wengine walipe gharama ya mapambano ndipo wewe ujitokeze kudai sehemu ya ushindi.
Na hili ulitie moyoni, ulitie akilini, ulitie katika kumbukumbu zako:
MABADILIKO TANZANIA YATATOKEA!
Ukiwa pamoja nayo, yatatokea.
Ukiwa kinyume nayo, yatatokea.
Ukiwa kimya, yatatokea.
Ukiwa mbele, yatatokea.
Ukiwa nyuma, yatatokea.
NA WEWE AU BILA WEWE, LAZIMA YATOKEE!
Unaweza kuchelewesha mapambazuko, lakini huwezi kulizuia jua kuchomoza.
Unaweza kuzuia mto kwa muda, lakini huwezi kuyaamuru maji yaache kutafuta njia.
Unaweza kuwakandamiza watu, lakini huwezi kuizika milele kiu yao ya haki na uhuru.
Na siku historia itakapofungua kurasa zake, haitauliza ulikuwa na cheo gani, ulikuwa karibu na nani, au ulikuwa na mali kiasi gani.
Itauliza ulisimama wapi wakati watu walipokuwa wakidai haki zao.
Itauliza ulisema nini wakati wengine waliponyamazishwa.
Itauliza ulifanya nini wakati kusimama upande wa haki kulipokuwa na gharama.
KUMBUKA: HISTORIA HAIANDIKWI TU NA WALE WALIOSHINDA, BALI PIA NA WALE WALIOKUWA NA UJASIRI WA KUSIMAMA WAKATI WENGINE WALIPOCHAGUA KUNYAMAZA.
SIMAMA, UHESABIWE!
MAANA MABADILIKO YATATOKEA, NA WEWE AU BILA WEWE
Buddy retweeted
Leo umetimia mwaka mmoja tangu mauaji yaliyofanywa kwa makusudi na vyombo vya dola vya Tanzania dhidi ya Watanzania wasio na hatia.
Mauaji ya October 2025 yalikua yanaweza kuepukika na uchaguzi ukafanyika kwa amani na usalama.
Kwasababu ya kiburi na uchu wa madaraka watawala waliamua kupuuza wito wa mda mrefu wa viongozi wa dini, vyama vya siasa, mashirika yasiyo ya kiserikali na hata watu maarufu ya kutaka mabadiliko ya katiba na sheria za uchaguzi ili kuwezesha uchaguzi huru na haki.
Mpaka sasa mwaka mmoja baadae Nchi iko kwenye mkwamo mkubwa wa kisiasa, watu wanaendelea kutekwa, kuuawawa na kupotezwa.
Kila anaetoa sauti ya kukemea uovu na kutaka maridhiano na uwajibikaji wa kweli anakabiliwa na kifo au mashitaka ya uongo.
Inaonekana hawa watawala wameshindwa kujifunza kwa yale mabaya yaliyotokea, Inaonekana wanafurahia kuendeleza utawala wa mkono wa chuma, udikteta na ubabe, mauaji, utekaji na kunyamazisha badala ya kushawishi na kutatua matatizo.
Kwa kutumia njia hizi mbele ni giza tupu, hakuna sehemu ambayo utawala wa kibabe Umefanikiwa kunyamazisha watu wote, Nchi hii ina watu zaidi ya milioni 70, hakuna siku watu wote hawa watanyamazishwa kwa uongo na kikundi kidogo cha watu kwa kutumia ubabe.
Njia pekee ya kutatua mkwamo huu ni.
1. Kumuachia Mwenyekiti Lissu na kufuta kesi za uongo dhidi ya wanachama wetu wote.
2. Kuachia mateka wote na kusitisha utekaji na mauaji ya kiholela.
3. Kuruhusu msuluhishi huru (mediator) kuleta watu pamoja na kuzungumza kwa ukweli na uwazi.
4.Uwajibikaji bila upendeleo kwa wahusika wa mauaji, kulipa fidia familia za wahanga, kutibu majeruhi wote na kuwapa fidia.
5. Kuruhusu Uchunguzi huru na kuomba radhi mbele ya Watanzania kwa makosa makubwa yaliyofanywa na vyombo vya dola dhidi ya raia wake.
6. Kuandika katiba mpya ya Nchi na sheria za uchaguzi ambazo zitarudisha umoja na haki kwa kila mtu.
7. Kutamka kwa uwazi kwamba makosa kama yale hayatajirudia tena kwenye Nchi yetu.
8. Kuhakikisha familia zinapata miili ya wapendwa wao na kufanya maziko ya heshima, kiafrika na kidini.
Kuendelea kutumia ubabe ni kuchochea chuki, uhasama na visasi kwa siku zinajazo…
Watawala badala ya kutumia chawa na ubabe kujaribu kuhujumu Chadema na uongozi wa Chadema, Tumia busara kufanya jambo sahihi la kuponya Nchi hii.
Tunajua mipango yenu dhidi yetu, lakini haki haijawahi kushindwa.
Endeleeni kupumzika kwa amani wote mliouwawa kikatili na kibabe, poleni majeruhi na wahanga wote.
Haki inaweza kuchelewa Lakini haki itapatikana tu.
Buddy retweeted
Tusambaze huu ujumbe kwa REPOST ZA KUTOSHA labda wakenya watatuelewa.
#FreeTwahaMwaipaya
Buddy retweeted
“Wahe Majaji, mzigo ambao mmekabidhiwa mabegani mwenu ni kuamua kama,
kwa ushahidi huu, kuna uhaini. Kama mkiona kuna uhaini you should not hesitate to convict & punish me appropriately. Msiogope. Kama mkiona hakuna uhaini, msiogope kuniachia huru.” - Tundu Lissu 28.09.2026.
Buddy retweeted
Tundu Lissu ni mtu mwenye akili mingi aliyezaliwa ndani ya Taifa lenye WAPUMBAVU wengi. Mungu huleta watu wa aina yake kwenye Taifa kama letu ili ku BALANCE mambo. Hawa watu wakikosekana, watu ndani ya Taifa husika huishi kama WANYAMA.
Buddy retweeted
“Nimepigania haki na demokrasia kwa sehemu kubwa ya maisha yangu. Msimamo huo umenigharimu sana. Umeniletea madhila mengi sana. Msimamo huo, kwa siku zilizobaki za maisha yangu, nitaendelea kuusimamia, na kama ikibidi kuufia, nipo tayari kufa.” — Tundu Lissu, 28.09.2026
Buddy retweeted
*MANENO YA MWISHO YA TUNDU LISU, leo:*
“Waheshimiwa Majaji miaka 60 iliyopita, kuna mhaini mwingine alifungwa kifungo cha maisha nchini Afrika Kusini, kabla hajahukumiwa alisema maneno yafuatayo ambayo naomba kuyafanya yawe maneno yangu leo, "I have fought against white domination and I have fought against blood domination, and my Lords, it is an ideal I am prepared to die for"
Nimepigania haki na demokrasia kwa sehemu kubwa, kuwa na nchi ya demokrasia, imekuwa ni ideal kwa nchi yangu, msimamo huo umenigharimu sana, umeniletea madhira mengi sana, msimamo huo kwa siku zilizobaki kwa maisha yangu ni msimamo ambao nitaendelea kuusimamia, na kama ikibidi kufa ni msimamo ambao nipo tayari kufa.
Namalziia kwa neno moja:
waheshimiwa majaji, kosa la uhaini halina kosa dogo, halina kosa ambalo ukishindwa kuthibitisha uhaini unahukumu kwa kosa dogo, it is either death sentence or acquittal, hakuna kakosa kadogo kwenye uhaini, waheshimiwa majaji, mzigo ambao mmekabidhiwa mabegani mwenu ni
kuamua kama kwa ushahdii huu kuna uhaini, kama mkiona kuna uhaini you should not hesitate to convict and punish me appropriately, do not hesitate, msiogope, kama mtaona kuna uhaini msiogope kunihukumu, kama mkiona hamna uhaini
msiogope kuniachia huru.
You have God before you, msije mkaletewa maneno kuna kosa dogo, hakuna kosa dogo kwenye uhaini, if the evidence doesn't fit— acquit, huo ni mzigo ambao ni wa kwenu peke yenu waheshimiwa majaji. Nimemaliza”
Tundu Antiphas Lissu, September 28, 2026. Mahakama Kuu, Dar.
Buddy retweeted
No storm of persecution can silence a voice that refuses to surrender.
Unyielding.
Fearless.
Indomitable.
SC Tundu AM Lissu. 🇹🇿
Buddy retweeted
Tundu Lissu. The man, the myth, the legend.
Leo Mahakama Kuu, Tundu A.M Lissu alikuwa anawasilisha hoja za mwisho za utetezi katika kesi ya uhaini inayomkabili aliyoshtakiwa na Jamhuri.
Tundu Lissu ametumia jumla ya dakika 349 kuwasilisha final submission yake kwa siku ya leo pekee na bado hajamaliza hoja zake zote.
Tundu Lissu ameanza kuwasilisha hoja zake kutoka saa 9:30 asubuhi hadi saa 13:32 mchana ambazo ni jumla ya dakika 242 (sawa na saa 4 na dakika 2).
Halafu, akarejea mchana baada ya kutoka health break. Kutoka saa 15:24 alasiri hadi saa 17:11 jioni ni jumla ya dakika 107 (sawa na saa 1 na dakika 47).
Kumbuka, Tundu Lissu anasimama dakika zote akiwa na majeraha ya kutisha ya risasi mwilini kwake, oparesheni 21 na risasi nyingine mgongoni.
Anyways, bado TAL hajamaliza final submission yake. Tutaendelea kesho na kwa kuwa hukumu ya kesi hii ni kunyongwa hadi kufa TAL amesema
“Kwa kuwa adhabu ya hukumu katika kesi hii ni kifo, mimi nitajitetea kwa kila kitu nilichonacho. I will defend myself with everything I’ve in my books”
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.
Buddy retweeted
Tumuombe Mungu Juu ya Uzima
na Afya kwa TAL! Tumtakie heri leo akihitimisha safari ya utetezi kwa kufanya majumuisho ya mwisho (Final Submission).
Buddy retweeted
Mapokezi ya JOHN HECHE Shinyanga sio poa Bro.
Hapa watu wanasherekea mengi. Lakini kikubwa ni kwamba wanafurahia CHADEMA ikiongozwa na LISSU akiwa Gerezani na Heche akiwa nje bado wapo imara hawajawasaliti watanzania.
Madai yetu watanzania YANAJULIKA, TUMEKATAA SIASA ZA MASAJI.
Repost 200
Buddy retweeted
Uadilifu wa Mhe. Tundu Lissu haupimwi kwenye kijiko wala haujawahi kutiliwa mashaka na watanzania
Buddy retweeted
Mkutano wangu na waandishi wa habari niliokuwa nifanye katika Hotel ya Golden Tulip nimeuahirisha.
Nimesikiliza hotuba za Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu. Wameeleza vizuri kuhusu uvumi na upotoshaji uliokuwa ukifanyika juu yangu na misimamo juu ya chama chetu.
Nimedumu katika mapambano haya kwa zaidi ya miaka 22. Nimeenda lock-up zaidi ya mara 50. Nimezunguka nchi hii usiku na zaidi ya mara tatu. Nimewahi kuwa magerezani mara kadhaa, nimekoswa kuuawa zaidi ya mara tatu, na nimewahi kukimbia nchi.
Katika yote haya, nimekuwa nikitoa sadaka kubwa kwa ajili ya mapambano haya, ikiwemo ku-sacrifice familia yangu mara zote.
Kazi hii kwangu si ajira, si cheo, wala si njia ya kujitafutia maslahi. Ni huduma. Ni wito. Ni kama injili ninayoamini na kuitumikia.
Kwa hiyo, siwezi kuruhusu uvumi, upotoshaji au tafsiri za watu kuniondoa kwenye misingi ambayo nimeisimamia kwa zaidi ya miongo miwili.
Nitakuwa kwenye mapambano haya kwa imani, ujasiri na dhamira njema siku zote.
Buddy retweeted
Tundu Lissu; Kila mara panapokuwa na ukandamizaji wa haki za Wananchi nimejitahidi kuwa sehemu ya mapambano ya Wananchi hao ya kupinga huo ukandamizaji.
Kauli mbiu yangu waheshimiwa Majaji (My moto) Upinzani dhidi ya Ukandamizaji ni utiifu kwa Mungu (Resistance to Oppression is obedience to God).
Msimamo wa maisha yangu haya umekuwa na gharama kubwa sana kwangu
Buddy retweeted
Wananchi tuna deni kubwa sana tunalodaiwa na Tundu Lissu!
Lakini hebu tujiulize kwa unyoofu kabisa: Tundu Lissu anajitoa kwa ajili ya nani? Anajitoa kwa ajili yake? Familia yake? Anatafuta fedha, uteuzi au cheo?
Kama angeamua kuwa mwanasiasa wa maigizo na kujali tumbo lake, angeendelea kusimama kwenye msimamo huu? Angeendelea kubeba gharama kubwa kiasi hiki, gharama inayoweza hata kukatisha uhai wake?
Juzi, Agosti 21, 2026, Mahakama Kuu imeamua kwamba Tundu Lissu ana kesi ya kujibu katika shauri la uhaini, hatua inayompeleka katika hatua ya utetezi.
Lakini sasa swali si Lissu pekee. Swali ni sisi tulioko nje ya gereza.
Je, kweli tunaguswa na yale anayopitia? Je, tunayaishi yale anayoyapigania? Je, tunathamini uhuru, haki, Katiba bora na utawala wa sheria kwa kiwango kinachostahili gharama anayolipa?
Inaumiza kuona mtu mmoja akibeba mzigo mzito wa mapambano, wakati sisi tuko busy na udaku, maigizo ya "machawa" na wasanii waliopotea njia kwenye muziki na filamu, porojo za mitandaoni na soka letu la mchangani lisilo na mbele wala nyuma!
Tuna muda wa kujadili kila kitu, lakini hatuna muda wa kujadili maisha yetu wenyewe! Hili si suala la kumpenda Lissu. Ni suala la kujiuliza kama tunathamini kile anachokipigania. Kwa sababu kama mtu anajitoa mhanga kupigania haki zetu, lakini sisi tunaishi kana kwamba hakuna kinachoendelea, basi kuna pengo kubwa kati ya gharama anayolipa yeye anayepigania haki na thamani tunayoweka sisi tunaotetewa.
Na kama Tundu Lissu, mwanasheria mbobevu anayejua vizuri nguvu na udhaifu wa sheria, anaweza kufikishwa kwenye hali hii, basi tujiulize: Itakuwaje kwa mwananchi wa kawaida asiye na jina, fedha, uelewa wa sheria wala uwezo wa kupata msaada wa kisheria?!
Huenda siku moja tukaja kugundua kwamba tulikuwa na mtu aliyekuwa tayari kupoteza uhuru wake na hata maisha yake kwa ajili ya misingi aliyoiamini, lakini sisi tulipoteza muda wetu tukishangilia vitu ambavyo havibadili chochote katika maisha yetu.
Lissu anaweza kuwa gerezani, lakini swali kubwa zaidi ni: dhamira yetu iko wapi?!
Tusiishie tu kumshangilia mtu anayeteseka kwa ajili yetu. Tujiulize tunafanya nini ili maumivu anayoyapitia yasiwe yake peke yake.




















