Pinned Tweet
mother’s love knows no bounds, and neither does her grief. For a year now, the family of Humphrey Polepole has endured "untold sorrow," looking for the truth behind his violent disappearance from Dar es Salaam. No family should have to carry this heavy burden of silence.
As a widow who sacrificed everything to raise her children alone, Annamary Polepole never imagined facing a reality where her children would be taken. A year after Humphrey’s abduction, his family continues to search for peace, closure, and basic human dignity. 🕊️🌿#freehpolepole@ipu @hrw @UNGeneva @UPRinfo @SenTedCruz @SenatorShaheen @commonwealthsec @EUparliament @EPPGroup @ecrgroup @WHO @ilo
Tanzanite retweeted
On the first anniversary of Tanzania’s sham elections, the brutal repression of political opposition and continued arbitrary detention of our client @TunduALissu expose the authorities’ contempt for their own people. The Commonwealth can no longer stand by. It must take decisive action against Tanzania’s government.
Tanzanite retweeted
Kesi imefunguliwa wiki hii
Imepangiwa Jaji Wiki hii
Imesikilizwa pande zote mbili wiki hii
Uamuzi umetoka wiki hii
Utekelezaji unapaswa kuanza wiki hii
Mkiambiwa wenzenu wamewazidi mnaanza kulalamika!
Mahakama zenu zinaweza kutoa haki kwa wakati?
#FreeTwahaMwaipaya
Tanzanite retweeted
“Samahani sauti iligoma”
Vile watu wengine walikodoa macho hapo wanasema kimoyomoyo “please God! Iwe leo!”
Yaani damu za watu zinanena!!
Hapa hata wamtoe nani kafara hawatoboi!!!@USAmbTanzania @hrw @ICC @usembassytz @UN @tedcruz @SenTedCruz @SenWarren
Tanzanite retweeted
Naingia kulala naomba niwaache na hii clip…..
1. Zingatia “Huyo mtu wa kati aliekuwa anafanya huo uratibu ”. Yani dalali.
Kelele zote alizopiga kwa Zitto, na yeye kaishia kufanya kile kile.
2. Zingatia alipewa nauli na gharama za huko Dar, Sasa connect dots na issue ya sea cliff.
I think mpaka sasa nchi nzima inajua huyo “Mtu wa kati” ni Godbless Lema.
Kuna siku hii familia itamtaja kwa jina…..
Nna swali, Chadema kama chama walitoa ahadi na msimamo kwa wananchi kuwa hawatopiga magoti kwa wauwaji, sasa imebainika kuwa mmoja wao anafanya kazi na wauwaji na alijaribu kuishawishi familia ya Lissu ikapige magoti kwa wauwaji, hatua gani zitachukuliwa???
Pia wananchi inabidi wampige marufuku Lema kutaja jina la Lissu kuanzia Leo. Anatumia mateso ya Lissu kuhalalisha usaliti wake.
Lissu kasema hadharani, hataki huruma anataka haki, Lema why anafosi kufanya kitu Lissu amekikataa? Yeye ndio anampenda sana Lissu kuliko sisi?? Wasaliti waache kumtumia Lissu kwenye ushetani wao.
Moja ya somo tulilopata kwenye hili sakata, dada yenu siwezi kuongea vitu sensitive au kuongea jambo la kumchafua mtu bila kuwa na uhakika wa 100%. Imagine inteview zote zilizofanywa ili nionekane muongo kwa wananchi na Lema aonekane sio msaliti ila leo Mungu kawaonyesha Watanzania dada yao waliemwamini miaka yote hajabadilika.
Tanzanite retweeted
Wataalamu wa UN Walaani Kutokuwepo kwa Haki kwa Waathiriwa wa Ghasia Tanzania
Wataalamu wa Umoja wa Mataifa (UN) wameeleza wasiwasi mkubwa kuhusu kutotolewa kwa ripoti kamili ya Tume ya Uchunguzi wa ghasia zilizotokea Tanzania wakati wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025, mwaka mmoja baada ya matukio hayo.
Wamesema mamia ya waathiriwa wa mauaji, kupotezwa kwa lazima, kukamatwa kiholela na mateso bado hawajapata haki, huku hakuna maafisa wa serikali walioshtakiwa kuhusiana na ghasia hizo.
Wataalamu hao wameitaka serikali ya Tanzania kuchapisha ripoti hiyo bila kuchelewa, pamoja na kufanya uchunguzi huru na wa haki ili kuhakikisha waathiriwa wanapata ukweli, haki na fidia.
Aidha, wameeleza wasiwasi kuhusu madai ya kuendelea kwa ukandamizaji dhidi ya waandishi wa habari, wanaharakati na wapinzani wa kisiasa.
Kauli hiyo pia imegusia hali ya kiongozi wa upinzani, Tundu Antipas Lissu, ambaye amekuwa rumande tangu Aprili 2025 akikabiliwa na mashtaka ya uhaini, huku akitarajia hukumu ya mahakama Novemba 6, 2026.
Tanzanite retweeted
Msiwe na Hofu Mungu anajibu,
amewaonyesha ishara ila wamekuwa na shingo ngumu, lakini ishara zote zipo ameshawaonyesha
wamefanywa kuwa na shindo ngumu ili wafutwe wote #Mo29
Tanzanite retweeted
Marking one year since the bloodbath and massacre of the Tanzanian people following the 29th October 2025 general elections.
The government of @SuluhuSamia unleashee terror and killed thousands of Tanzanians whose only mistake was to call for justice and free elections.
Tanzanite retweeted
Human Rights Defenders from Kenya have today held a vigil, standing in solidarity with the people of Tanzania as they demand justice for Tanzanians killed on the 29th of October 2025 by Samia's killer militia. #FreeAllPoliticalPrisoners #PASNet #FreeTunduLissu #SamiaMustGo
Tanzanite retweeted
The Kenya National Commission on Human Rights (KNCHR) has condemned the alleged abduction of Tanzanian political activist Twaha Salim Mwaipaya in Machakos County on October 25, saying his disappearance raises concerns about the safety of dissidents and refugees in Kenya.
standardmedia.co.ke/crime-an…
Tanzanite retweeted
Leo ndo siku ya kupigia mstari kuwa hatuna serekali,au tuna serekali haramu.
Balozi mbali mbali nchini Tanzania na high commission zinaomboleza mpaka kushusha bendera nusu mlingoti Ila serekali haijulikani ilipo!!😢
Leo ndo siku ya kupigia mstari kuwa hatuna serekali,au tuna serekali haramu.
Balozi mbali mbali nchini Tanzania na high commission zinaomboleza mpaka kushusha bendera nusu mlingoti Ila serekali haijulikani ilipo!!😢
Tanzanite retweeted
Video ya kwanza ilirekodiwa na wanajeshi, angalia mwishoni utaona mwanajeshi na mabuti yake.
Wanajeshi waliorekodi video walinitumia huku wanalia machozi.
Video ya pili mpaka waislam waliuawa ila leo Bakwata ipo kimya.
Tanzanite retweeted
29.10.2026. SIKU YA MAOMBOLEZO YA KITAIFA. SIKU YA KUJITATHMINI NA KUJISAHIHISHA.
Nilianza kumbukizi hii kwa kusali Misa Takatifu asubuhi katika kanisa langu la Mtakatifu Martha, Mikocheni. Baadaye nikashiriki mazungumzo na Jenerali Ulimwengu kupitia Post:
youtube.com/live/lTdENudIxCc…
Sasa napenda kutoa ujumbe wangu kuhusu siku hii, maana yake kwa Taifa letu na nini kifanyike ili tutoke katika mkwamo unaotukabili.
1. TUKUBALI MSIBA ULIOLIPATA TAIFA.
Takwimu za Tume ya Rais iliyoongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman: vifo 518, wakiwemo raia 502 na maafisa wa vyombo vya ulinzi na usalama 16. Watoto 21 walipoteza maisha. Tume yenyewe ilitahadharisha kuwa idadi hii inaweza isiwe ya mwisho.
Huu ulikuwa msiba wa Taifa, bila kujali tofauti zetu za kisiasa. Kila uhai una thamani.
2. POLE KWA WAHANGA WOTE.
Familia zilizopoteza wapendwa wao, watoto waliobaki yatima, wajane, wagane, majeruhi na wote walioathirika.
Nyuma ya kila takwimu kuna binadamu, familia na matumaini yaliyokatizwa. Kwa wote waliofiwa nasema: Hatujawasahau. Machungu yenu ni machungu yetu sote.
3. KWA NINI TUIKUMBUKE OKTOBA 29?
Tume ya Chande ukurasa wa 52 wa hotuba ya Mwenyekiti wake ilipendekeza:
“..Serikali kutenga siku ya Maombolezo ya Kitaifa kuwakumbuka Watanzania zaidi ya 500 waliofariki kwenye ghasia za wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025;”
Bado tunaisubiri Serikali itangaze siku rasmi ya maombolezo. THRDC imependekeza tarehe 29 Oktoba iwe siku ya kumbukizi ya kila mwaka, na viongozi wa dini wamehimiza sala na tafakari.
Kwa hiyo, tunapoitumia siku ya leo kuomboleza, tunafanya hivyo kwa nia njema, kuonesha mshikamano na kuwafariji wahanga wasije wakadhani Taifa limewasahau.
4. TUELEWE CHANZO CHA MGOGORO, SI VICHOCHEO PEKEE.
Tume ya Chande ilitofautisha kati ya vyanzo vya ghasia na vichocheo vyake. Vyanzo ni kama mafuta, vichocheo ni kama kiberiti.
Ilitaja vyanzo vitano: matatizo ya kisiasa na madai ya Katiba Mpya na mageuzi ya uchaguzi; ugumu wa maisha, ajira na fursa za kiuchumi; matatizo ya kijamii, rushwa na utekaji; udhaifu wa utendaji wa taasisi za umma; na changamoto za mahusiano ya kimataifa.
Tume ilijadili pia vichocheo, vikiwemo kauli za baadhi ya wanasiasa na matumizi ya mitandao ya kijamii.
Hata tukidhibiti vichocheo, hatutakuwa tumetatua tatizo kama mafuta yataendelea kuwepo.
Ndiyo maana nimekuwa nikisisitiza umuhimu wa kutekeleza kwa vitendo falsafa ya Rais Samia ya 4Rs: Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi na Kujenga Upya. Vijana wanahitaji kusikilizwa. Malalamiko yao yashughulikiwe, huku kila mmoja akiheshimu sheria na haki za wengine.
TUTOKEJE KATIKA MKWAMO HUU?
Ninapendekeza hatua zifuatazo:
Serikali itoe msimamo kuhusu siku rasmi ya maombolezo iliyopendekezwa na Tume ya Chande.
Wahanga wote wabainishwe, wafikiwe na kusaidiwa kulingana na mahitaji yao halisi.
Uchunguzi huru wa matukio yenye viashiria vya jinai, mauaji na utekaji ufanyike, na wahusika wawajibishwe kwa mujibu wa sheria.
Mapendekezo ya Tume kuhusu Katiba Mpya, mageuzi ya uchaguzi, uwajibikaji wa taasisi na maridhiano yafanyiwe kazi.
Wazee, viongozi wa dini, wanawake na vijana washirikishwe kikamilifu katika kujenga uelewano wa kitaifa.
Maridhiano si kufuta ukweli, kusahau wahanga au kuacha kuwajibisha waliovunja sheria. Maridhiano ni kuwa na ujasiri wa kukiri mapungufu, kutenda haki, kurekebisha makosa na kujenga upya imani ya wananchi katika taasisi zao.
Ndugu zangu Watanzania, Oktoba 29 isiwe siku ya kuchochea visasi. Iwe siku ya kujitathmini na kujisahihisha, kuthamini uhai wa binadamu na kujiwekea dhamira kwamba madhila haya hayatatokea tena.
Tusisahau waliopoteza maisha. Tusiwaache wahanga peke yao. Tusifanye hofu kuwa mbadala wa amani.
TUKUMBUKE. TUJITAFAKARI. TUJISAHIHISHE. TUTENDE HAKI. TUPONYE MAJERAHA. TURIDHIANE NA TUSONGE MBELE KAMA TAIFA MOJA.
Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, awafariji wafiwa, awaponye majeruhi na alijalie Taifa letu amani ya kweli, amani yenye haki.
Amina.
Tanzanite retweeted
MAREKANI: VIFO VYA UCHAGUZI TANZANIA HAVITAFAGILIWA CHINI YA KAPETI
Oktoba 29, 2026
Balozi wa Marekani nchini Tanzania amesema vifo vilivyotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 havitasahaulika wala kufichwa, akisisitiza umuhimu wa uwajibikaji na majibu kwa familia zilizopoteza wapendwa wao.
Katika ujumbe wake wa leo, balozi huyo amesema jumuiya ya Ubalozi wa Marekani imeungana kuwakumbuka wote waliopoteza maisha katika vurugu hizo, pamoja na familia zinazoendelea kuomboleza na kutafuta majibu.
Kauli hiyo inarejea msimamo alioutoa mbele ya Seneti ya Marekani wakati wa kusikilizwa kwa uthibitisho wa uteuzi wake, akisisitiza kuwa suala hilo halitafagiliwa chini ya kapeti.
Kauli hiyo inaashiria kuwa matukio ya uchaguzi wa Oktoba 2025 yanaendelea kuwa sehemu ya mjadala kuhusu uwajibikaji, haki za binadamu na mustakabali wa uhusiano kati ya Marekani na Tanzania.
Hata hivyo, familia zilizopoteza wapendwa wao bado zinahitaji majibu kuhusu mazingira ya vifo hivyo na hatua zinazochukuliwa kuhakikisha uwajibikaji.

















