Pinned Tweet
JE UNAJUA KWA NINI HUFANIKIWI?
Una mizigo mingi isiyo ya lazima wala faida ambayo umeibeba:-
1.Umejipa jukumu la kuwa "mpelelezi" wa maisha ya wengine na umesahau maisha yako.
2.Umebeba vinyongo na visasi moyoni vinavyokufanya uwafikirie waliokuumiza zaidi kuliko kufikiria furaha na maendeleo yako.
3. Una marafiki wengi ambao ni kama kupe, wapo kukutumia tu na hawachangii lolote katika maendeleo zaidi ya kujifanya ndio watu wako karibu lakini kumbe wapo kwa maslahi yao!
4.Umeweka mbele zaidi "watu watanichukuliaje" kuliko kuangalia maisha yako.Watu ndio wanakuchagulia aina ya maisha unayoishi na unajilazimisha kuishi kama wao hata kama huna uwezo huo.
5.Unaongea zaidi ya kasuku lakini vitendo hakuna.Unatamani mafanikio tu moyoni lakini huna mipango ya kuyafikia.
6.Maisha yako yote umeyaweka kwenye mitandao ya kijamii.Huna siri hata moja!Hivyo unalazimika kuishi aina ya maisha ambayo yataendelea kufanana na yale uliyoyaweka kwenye mitandao ya jamii kwa sababu ukibadilika tu watasema "umefulia"
7.Kila aliefanikiwa ni rafiki yako au utasema ni mtu wako wa karibu na unaishia kuwasifia tu na kupiga nao picha lakini hujifunzi kutokana na mafanikio yao na wala hutumii fursa hiyo ya kujuana nao.
8.Upo sahihi kila siku(you are always right). Huambiliki, hushauriki na kila wazo atakalotoa mwenzako basi si zuri ila la kwako ndio sahihi na utataka litekelezwe hilo hilo. Mwisho wa siku kila mtu anakukimbia hakuna wa kukuambia "hapa umekosea" kwa sababu ya ujuaji wako.
9.Hujifunzi maarifa mapya.Mara ya mwisho kusoma kitabu ilikuwa ni "Ngoswe, penzi kitovu cha uzembe" Tena ni kwa sababu ilikuwa ni kwa ajili ya kujibia mtihani. Hujifunzi "life skills" wala ujuzi mwingine.
10.Unazurura mno mitandaoni bila faida. Kwako wewe intaneti ni kwa ajili ya kuchati tu na kufuatilia habari za mjini ambazo tangu umeanza kuzifuatilia hujawahi kuingiza hata shilingi moja, zaidi unateketeza tu hela yako ya vocha.
ISHUSHE hiyo mizigo kama kweli inahitaji kusonga mbele!
Zee BabaLao retweeted
Hakuna mambo ya "Mwakani", zawadi ziko hapa sasa hivi ๐
Kila unachonunua msimu huu wa sikukuu, hakikisha unalipa kwa TemboCard VISA. Yaani sio tu kwamba unafanya manunuzi kwa urahisi na usalama, bali pia unajiongezea nafasi ya kuondoka na Mkwanja kila wiki, kila mwezi mpaka mwisho wa mwaka!
#kilamtuapatenatembocardvisa
Zee BabaLao retweeted
Huyu Ni Tapeli Tu
๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐! ๐
Yanga players have already been informed of Fadlu Davidsโ imminent arrival.
During this international break, Yanga will travel to Zanzibar for a short training camp to prepare for their upcoming matches and the CAF Champions League group stage.
Fadlu Davids will lead the team to Zanzibar on Sunday.
A new era begins at Jangwani! ๐น๐ฟ
Mashabiki wa Yanga, mnajisikiaje kuhusu sura hii mpya? ๐
#AfricanFootball #Yanga
Zee BabaLao retweeted
Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa kwenye mazungumzo na Mhe. Noluthando Mayende-Malepe, Balozi wa Afrika Kusini anayemaliza muda wake nchini Tanzania, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 06 Novemba, 2026.
Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa kwenye picha na Mhe. Noluthando Mayende-Malepe, Balozi wa Afrika Kusini anayemaliza muda wake nchini Tanzania, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 06 Novemba, 2026.
Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa kwenye mazungumzo na Mhe. Noluthando Mayende-Malepe, Balozi wa Afrika Kusini anayemaliza muda wake nchini Tanzania, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 06 Novemba, 2026.
Zee BabaLao retweeted
BULEMBO AIBANA SERIKALI SUALA LA AJIRA KWA WAHITIMU, WAZIRI MKUU ATOA KAULI RASMI
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema Serikali inaendelea kulifanyia kazi suala la ajira kwa wahitimu wa vyuo vikuu kupitia hatua mbalimbali za kibajeti, kisera na kiutawala, akieleza kuwa suala hilo ni muhimu kutokana na changamoto inayowakabili vijana wengi nchini.
Dkt. Nchemba ameyasema hayo leo Alhamisi Novemba 05, 2026 wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum kupitia kundi la Vijana, Halima Bulembo, aliyetaka kujua mkakati wa Serikali kuhakikisha mafunzo kwa vitendo yanayotolewa kwa wahitimu yanakuwa daraja la kupata ajira zenye staha na endelevu.
Waziri Mkuu amesema hoja hiyo ni ya msingi na inafanana na hoja binafsi iliyowahi kuwasilishwa na Mbunge Dkt. Selemani Jafo, ambayo Serikali iliipokea na kuanza kuifanyia kazi.
Ameeleza kuwa Serikali itaendelea kulifanyia kazi suala hilo na kutoa taarifa kuhusu hatua zitakazokamilishwa, ikiwemo kutoa maelezo Bungeni pale itakapohitajika.
Katika swali lake, Bulembo amesema takribani asilimia 62 ya wahitimu wa vyuo vikuu nchini hutumia muda mrefu kupata ajira rasmi, akitaka kujua namna Serikali itakavyotekeleza dhamira iliyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025โ2030 ya kuwapatia wahitimu mafunzo kwa vitendo kupitia taasisi za umma na sekta binafsi.
Amehoji pia hatua zitakazochukuliwa kuhakikisha waajiri wanatoa fursa hizo na kwamba mafunzo hayo yanawawezesha wahitimu kupata ajira badala ya kuwaongezea uzoefu bila uhakika wa kuajiriwa.
WAZIRI KAIRUKI ATOA ONYO KUHUSU UTAPELI, ULINZI WA TAARIFA BINAFSI MTANDAONI
Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari, Angellah Kairuki, amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ulinzi wa taarifa binafsi za wananchi na mifumo ya usalama wa mtandao ili kukabiliana na ongezeko la uhalifu na utapeli unaofanyika kupitia teknolojia ya kidijitali.
Akizungumza Bungeni jijini Dodoma leo Alhamisi Novemba 05, 2026 wakati akiwasilisha Mkataba wa Umoja wa Afrika kuhusu Usalama wa Mtandao na Ulinzi wa Taarifa Binafsi wa mwaka 2014, maarufu kama Mkataba wa Malabo, kwa ajili ya kuridhiwa, Waziri Kairuki amesema, ongezeko la matumizi ya mtandao linaambatana na kuongezeka kwa matishio ya usalama na makosa yanayofanyika katika mazingira ya kidijitali.
Ameongeza kwa kusema kuwa, mkataba huo unalenga kuimarisha ushirikiano baina ya nchi wanachama wa Umoja wa Afrika katika kukabiliana na uhalifu wa mtandao, ambao unaweza kufanyika katika nchi moja na kuathiri watu au mifumo ya nchi nyingine bila kuzuiwa na mipaka ya kijiografia.
โUsalama wa mtandao ni jambo muhimu sana katika ustawi wa taifa lolote duniani, na kwa kadri matumizi ya mtandao yanavyoongezeka, ndivyo ambavyo matishio ya usalama wa mtandao na makosa yanayofanyika kupitia mtandao yanavyozidi kuongezeka,โ alisema Kairuki.
Vilevile ameeleza kuwa, mkataba huo pia unaweka msisitizo katika kulinda faragha na taarifa binafsi za wananchi kwa kuhakikisha zinakusanywa, zinahifadhiwa na kutumika kwa kuzingatia misingi ya usiri na usalama, ili kuzuia matumizi yasiyoidhinishwa na ukiukwaji wa haki za watu.
โMkataba huu unaziwezesha nchi wanachama kushirikiana katika masuala ya usalama wa mtandao na ulinzi wa taarifa binafsi ili kufikia malengo ya kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika,โ alisema.
Ameendelea kwa kusema kuwa, Tanzania tayari ina mifumo ya kisheria inayosimamia eneo hilo, ikiwemo Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015, Sheria ya Miamala ya Kielektroniki ya mwaka 2015 na Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya mwaka 2022.
Mkataba huo unalenga kuimarisha zaidi ushirikiano wa kikanda na mifumo ya kisheria katika kuzuia na kukabiliana na makosa ya mtandao, pamoja na kuweka msingi wa uwajibikaji katika matumizi ya teknolojia.
































