ChabaSIR (@chabaSIR) header
ChabaSIR (@chabaSIR) profile picture

Author #AtasteofEastAfrica | | You enjoy reading? link below ⬇️

Joined August 2016
Photo by ChabaSIR (@chabaSIR)Photo by ChabaSIR (@chabaSIR)Photo by ChabaSIR (@chabaSIR)Photo by ChabaSIR (@chabaSIR)Photo by ChabaSIR (@chabaSIR)Photo by ChabaSIR (@chabaSIR)Photo by ChabaSIR (@chabaSIR)Photo by ChabaSIR (@chabaSIR)Photo by ChabaSIR (@chabaSIR)Photo by ChabaSIR (@chabaSIR)
The UN80 Reform Initiative is not so much about the WHAT and WHEN, but about HOW.
2
13
26
1,969
Today, I presented letters of credentials from Her Excellency @SuluhuSamia Suluhu, President of the United Republic of Tanzania, to His Excellency @antonioguterres, Secretary-General of the @UN introducing me as the new Permanent Representative of the United Republic of Tanzania to the United Nations. This marks the beginning of my tour of duty.
30
51
5
209
18,735
Balozi wa kudumu wa Tanzania 🇹🇿katika @UmojawaMataifa Togolani Edriss Mavura @tonytogolani hii leo amewasilisha rasmi hati ya utambulisho kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa 🇺🇳@AntonioGuterres jijini New York Marekani 🇺🇸 tayari kwa kuanza kazi. #HabarizaUN
7
20
1
68
3,883
Akipokea hati ya utambulisho kutoka kwa Mwakilishi wa kudumu wa 🇹🇿 katika @UN Balozi @tonytogolani Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa @antonioguterres ametoa pongezi kwa Tanzania kwa jinsi Baba wa Taifa hilo Hayati Mwl.Julius Nyerere alivyokuwa akipambania ukombozi wa Bara la Afrika
7
31
1
52
3,254
Generation shift and the twist of messaging between parents and teenagers is real. It was once talking to teenagers about how to navigate and survive in the cities, today it is about how to navigate and survive online! Dear My Darling Daughter Pearl, chaba-rhuwanya.medium.com/de…
7
21
1,608
A superb letter from a mother to a daughter turning 16 and gifted with a smartphone. Words so moving and lovely >>>>> Dear My Darling Daughter Pearl, chaba-rhuwanya.medium.com/de…
5
10
2,519
Ulikuwa mtu sahihi kuendesha Tume ya Taifa ya Mipango wakati huu tukitengeneza Dira ya Taifa ya 2050. Uliweza kuleta pamoja uzoefu wa Sekta Binafsi na Serikali, uliweza kuzungumza na ukaeleweka na Sekta Binafsi na kuzungumza na kueleweka na Serikali. Ulikuwa daraja. Ulikuwa mwangwi. Hatujajaaliwa watu wengi wa aina yako ndani ya Serikali. Kifo chako ni pigo kubwa kwetu sote tunaoamini katika ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi, na kumbukumbu yako itabaki nasi daima. Upumzike mahala pema Kaka @LNMafuru!
19
38
6
265
18,901
📍Seoul, Korea Kusini 🇹🇿🇰🇷 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. @SuluhuSamia akiwa amenyanyua juu vitabu vya  A Taste of East Africa mara baada ya kuvizindua wakati wa mkutano na Watanzania waishio Jamhuri ya Korea tarehe 05 Juni, 2024. Kushoto ni Mwandishi wa Kitabu hicho Chaba Mavura. 📸: IKULU
6
14
1,200
📍Korea 🇹🇿🇰🇷  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amenyanyua juu vitabu vya  A Taste of East Africa mara baada ya kuvizindua wakati wa mkutano na Watanzania waishio Jamhuri ya Korea tarehe 05 Juni,2024. Kushoto ni Mwandishi wa Kitabu hicho Chaba Mavura  📸:IKULU
1
8
22
2,792
Hayati Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi Hatumdai na Hatudai. Kiongozi rahimu, kiongozi jasiri, kiongozi mnyenyekevu, kiongozi muungwana, kiongozi mzazi na mlezi ndio sifa zinazomtambulisha Hayati Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyejaaliwa kuishi na kuona kizazi cha nne (Marais wanne) cha uongozi mbele yake. Hayati Rais Mwinyi ni kiongozi mwenye karama ya kipekee. Amekuwa Rais wa Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jambo ambalo ni nadra kutokea. Utulivu wake, urahimu wake na ujasiri wake, uliwezesha Zanzibar, na baadae Tanzania kuyaendea mageuzi makubwa ya kiuchumi na kisiasa. Katika nyakati zote, alipokea nchi katika mazingira magumu sana. Alikuwa Rais wa Zanzibar baada ya 'kuchafuka kwa hali ya siasa Zanzibar' na kujiuzulu kwa Hayati Rais Aboud Jumbe. Akawa Rais wa Tanzania akiipokea nchi ikiwa 'hoi bin taaban' kiuchumi, ikiwa haina bidhaa madukani, wala akiba ya fedha za kigeni. Katika nyakati zote mbili, alipokea dhima kwa unyenyekevu mkubwa, hakulaumu waliomtangulia, alilinda stara yao, na alifanya mageuzi makubwa bila kubeza yaliyokwishafanyika. Hayati Rais Mwinyi ameonyesha kuwa ujasiri na maamuzi magumu yanaweza kupatikana bila ya lugha kali, mkono wa chuma na kumwaga damu za watu. Alifungua uchumi wa Zanzibar, na akafungua uchumi na siasa za Tanzania. Ndiye aliyeruhusu uchumi wa soko kupitia 'Azimio la Zanzibar' na ndiye aliyeunda Tume ya Nyalali, kuruhusu Mfumo wa Vyama Vingi vya Siasa na kuruhusu Uhuru wa Habari na vyombo binafsi vya habari. Rais akaanza kuandikwa, kujadiliwa hadharani na hata kuzushiwa, wakati huo tukianza na gazeti la Motomoto. Hayati Rais Mwinyi anabaki kuwa kielelezo cha uwajibikaji nchini Tanzania. Alionyesha uwajibikaji kwa mfano alipojiuzulu bila shuruti wala manung'uniko baada ya kadhia ya mauaji kule Shinyanga. Wakati wa Urais wake, aliwahi kuvunja Baraza la Mawaziri kuonyesha kuwajibika kwa umma kutokana na tuhuma mbalimbali zilizoikabili Serikali yake. Hayati Rais Mwinyi alikuwa mwanademokrasia. Itakumbukwa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi baada ya kurejeshwa mfumo wa vyama vingi ulifanyika jijini Dar es Salaam, ukiwa ni uchaguzi mdogo wa Udiwani na mgombea wa upinzani Dkt. Masumbuko Lamwai wa NCCR akashinda na akatangazwa. Tukawa na diwani wa kwanza kutoka upinzani. Kwa upande wa diplomasia yetu, Hayati Rais Mwinyi alifanya mengi na makubwa ikiwemo kurejesha imani ya wawekezaji na wahisani wa maendeleo, kumalizia kiporo cha Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere cha ushiriki wetu kwenye harakati za ukombozi katika nchi za Namibia na Afrika Kusini, usuluhishi wa mgogoro wa Rwanda, kuirejesha Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, na kuanzisha mahusiano na Jamhuri ya Korea. Hayati Rais Ali Hassan Mwinyi atakumbukwa kwa busara na nukuu nyingi. Nitamkumbuka kwa nukuu yake aliyoitoa katika hotuba yake bora sana ya 'Twende na Wakati' aliyoitoa kwa Wazee wa Dar es Salaam akifafanua 'Azimio la Zanzibar'. Alisema, "Kama hatukwenda na wakati, kazi yetu itakuwa ni kufukuzia wakati - jambo ambalo hatulimudu. Tabia ya wakati ni kama ile ya bahari. Bahari inakupwa na kujaa mpaka ukingoni mwa maji. Baadaye maji hukupwa polepole, mpaka kufika wakati ikawa maji yote yamekwishaondoka ufukoni. Samaki werevu huondoka nayo hayo maji, yaani yakijaa huja nayo, yakitoka kutoka nayo, vinginevyo hupwelewa. Samaki watakaozembea kufuata maji watajikuta wamechelewa wanatapatapa juu ya mchango wakati maji hayo hayapo. Hiyo ndiyo maana ya kupwelewa". Maisha yake ni funzo kubwa kwetu sote. Ametuachia alama na sadaka zinazoishi. Ametuachia hadithi nzuri. Alikuwa mtu nadra. Amefariki siku nadra ya tarehe 29 Februari ambayo huja mara moja katika miaka minne. Hatudai. Hatumdai. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Hayati Mheshimiwa Rais Ali Hassan Mwinyi mahala pema peponi.
13
67
150
7,792
One of those writings that makes you pause and reflect! Then you remember the old adage that goes, 'until lions have their own historians, the story of the jungle will always glorifies men'. Women: Damn If We Are, Damn If We Aren’t! chaba-rhuwanya.medium.com/wo… Also found at thecitizen.co.tz/tanzania/op…
1
22
1
59
7,147
Women: Damned if we are, damned if we aren’t! fupi.co.tz/6x9bsCZ
3
1
7
3,261
Imekuwa ni miaka miwili ya Maridhiano ya kisiasa, Kujenga Uhimilivu, Mageuzi ya kiuchumi na kufuma upya Taifa letu. Pongezi Mheshimiwa Rais @SuluhuSamia kwa uongozi madhubuti, sera sahihi, na siasa safi. Kuongoza ni kulea. Umedhihirisha Mikono ya Mama ni mikono ya ulezi!
12
56
6
209
8,849
We were heartbroken to learn about the loss of about 149 lives during the Halloween festival in Seoul last night. We are joining you @President_KR and the people of Korea in mourning and grieving for this great loss. To those injured, we wish them a speedy healing and recovery.
314
314
17
2,810
Shukran za pekee kwa maafisa wetu wa Ubalozi wa Tanzania nchini Korea na makampuni ya utalii ya Zara Tanzania Adventures kutoka Tanzania Bara na Safanta Tours and Travels ma Choum Tours and Safari kutoka Zanzibar.
1
10
1
42
Kwa mara nyingine, ushiriki wetu katika maonyesho ya Utalii nchini Korea umefanikiwa kupata Tuzo. Safari hii Banda la Tanzania limepewa tuzo ya 'Best Booth Design' katika maonyesho ya Busan International Trade Fair. Nchi 33 zilishiriki na Tanzania ndio nchi pekee kutoka Afrika.
12
45
8
152
📍Seoul, Korea Kusini 🇹🇿|🇰🇷 Balozi wa Tanzania nchini Korea Mh. @tonytogolani akihutubia katika Hafla ya Uzinduzi wa Dira Mpya ya utendaji kazi wa Mfuko wa EDCF uliofanyika leo Julai 07, 2022, Jijini Seoul. Hafla hiyo imehudhuriwa na Viongozi wa Serikali ya ....⤵️ 📸: UBALOZI
1
7
22
The University of Cape Town (UCT) has introduced Swahili as an elective language course starting from 2023, said vice-chancellor Mamokgethi Phakeng in her opening address during the Africa Month panel discussion. sundayworld.co.za/education/…
3
26
1
63