Leo, Oktoba 19, 2026, nimeshiriki nikiwa mgeni rasmi katika hafla ya ufunguzi wa ofisi ya taasisi ya kusafirisha mahujaji ya Al-husna Hajj Trust Ltd (TAHUZA), iliyopo katika eneo la Masjid Omar Bin Al-Khattab, Msumbiji, Shehia ya Nyerere, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.
Leo Oktoba 19, 2026, nimefungua ofisi ya taasisi ya kusafirisha mahujaji ya Al-husna Hajj Trust Ltd (TAHUZA), iliyopo katika eneo la Masjid Omar Bin Al-Khattab, Msumbiji, Shehia ya Nyerere, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.
MWENYEKITI wa Taifa wa ACT Wazalendo, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, leo Ijumaa, tarehe 17 Julai 2026, amemtembelea Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jaji Joseph Sinde Warioba, katika makazi yake Mbezi Juu, Dar es Salaam.
Mheshimiwa Othman, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza Mstaafu wa Rais wa Zanzibar, alifika kwa lengo la kumjulia hali na kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali yenye umuhimu kwa taifa.
Habari Picha:
Mwenyekiti wa Taifa wa ACT Wazalendo, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, jana Alkhamis ya Julai 09 2026, amejumuika na Viongozi mbali mbali wa Kitaifa wa Serikali, Vyama vya Siasa, Dini, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na Wawakilishi wa taasisi mbalimbali, katika hafla ya uwasilishaji na utiaji saini wa Tamko la pamoja la Maridhiano ya kisiasa Zanzibar, huko katika Viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.
Leo Juni 05 2026, nimejumuika na Waumini wenzangu wa Kiislamu, katika Sala ya Ijumaa hapo Masjid As-Silm, Msikiti uliopo Bububu Kihinani, Mkoa wa Mjini-Magharibi Unguja.
Leo Mei 25 2026, nimepata fursa ya kujumuika na Mamia ya Waumini wa Kiislamu, pamoja na Wananchi wa Maeneo mbali mbali hapa Nchini, katika Maziko ya Marehemu Abdulghany Himid Msoma, (Coach Msoma), huko katika Makaburi ya Mwanakwerekwe Mjini Magharibi Unguja.
Nimeipokea kwa huzuni na masikitiko makubwa, taarifa ya kifo cha Ndugu yetu Bwana Abdulghany Himid Msoma, kilichotokea Mei 23 2026, akiwa matibabuni Nchini India.
Nachukua fursa hii kutoa salamu za pole kwa familia ya Marehemu, Ndugu, jamaa na marafiki.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amin!
Leo Mei 22 2026, nimejumuika na Waumini wenzangu wa Kiislamu katika Ibada ya Sala ya Ijumaa hapo Masjid Sunna, Msikiti uliopo Kikwajuni Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Leo Jumamosi ya Mei 16 2026, nimejumuika na wananchi na Viongozi mbali mbali wakiwemo, Wasomi na Wanataaluma Mashuhuri, Mabalozi na Wanadiplomasia Wanaowakilisha Mataifa yao mbali mbali hapa Nchini, Wawakilishi wa baadhi ya Vyama vya Siasa, Wahariri na Waandishi wa Habari Waandamizi, Viongozi wa Dini na Watu Maarufu, katika Kongamano Maalum la Mjadala wa Kitaifa kuhusu Mwelekeo na Khatma ya Nchi yetu, lililoandaliwa na chama chetu cha @ACTwazalendo na lililofanyika hapo katika Hoteli ya Serena, Jijini Dar es Salaam.
Leo Mei 03 2026, nimeshiriki na kuongoza nikiwa Mwenyekiti wa Kikao cha Kamati Kuu Maalum ya Chama chetu cha @ACTwazalendo, huko katika Ukumbi wa Hakainde Hichilema, uliopo ndani ya Jengo la Maalim Seif, Makao Makuu ya ACT Wazalendo, Magomeni Jijini Dar es Salaam.
Leo Aprili 26, 2026, nimepata fursa ya kuhudhuria nikiwa Mgeni Rasmi katika Kongamano la Ngome ya Vijana wa Chama chetu cha @ACTwazalendo, huko Wete Kaskazini Pemba, lililobeba maudhui ya " Uchumi wa Zanzibar ndani ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar" , ambalo limekuja sambamba na Maadhimisho ya Miaka 62 ya Muungano wa Tanzania.
Leo Aprili 25, 2026, nimepata fursa ya kuhudhuria nikiwa Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa mkutano mkuu wa jimbo la Pandani Kaskazini Pemba, ikiwa ni Uzinduzi rasmi wa mikutano mikuu ya majimbo ya Zanzibar, ambayo ni sehemu ya mikakati ya uimarishaji wa chama chetu cha @ACTwazalendo
Leo Aprili 13, 2026, nikiambatana na Mwenyekiti Mstaafu wa chama chetu cha @ACTwazalendo Ndugu Juma Duni Haji, tumekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola na Rais Mstaafu wa Malawi, @LAZARUSCHAKWERA.

















































