Mzeee thanks Again and Again kwa Shule Nzuri hii.
JAJI NDUNGURU AMEFANYA KOSA LA KIMKAKATI KWENYE MATUMIZI YA KESI YA ZOMBE ILI KUMFUNGA LISSU:
Akitoa adhabu, Jaji Dunstan Ndunguru lilirejea kesi ya kihistoria ya DPP dhidi ya ACP Abdallah Zombe na Wenzake 8 (Criminal Appeal No. 358 of 2013) ili kushusha shtaka kutoka UHAINI kwenda UCHOCHEZI.
Hata hivyo, Jaji Ndunguru alikiuka kwa MAKUSUDI misingi mikuu ya kesi hiyo ya Zombe katika maeneo yafuatayo:
1. KUGEUZA KOSA KI-OTOMATIKI BILA NOTISI (Haki ya Kusikilizwa).
Msimamo wa Kesi ya Zombe uko hivi:
Mahakama ya Rufani katika kesi ya Zombe ILISISITIZA kuwa matumizi ya vifungu vya 319(1) na (2) vya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA)—ambavyo vinaruhusu mahakama kumtia hatiani mshtakiwa kwa kosa dogo linaloendana na kosa kubwa (minor and cognate offence)—sio jambo la moja kwa moja au ki-otomatiki (not automatic).
Maana yake, mahakama haiwezi kugeuza kosa bila kumpa Lissu taarifa rasmi (notice) na nafasi ya kujitetea dhidi ya kosa hilo JIPYA.
KOSA LA JAJI: Ingawa Jaji Ndunguru alikiri kuwa kesi ya Zombe inakataza jambo hilo kuwa automatic, bado alihitimisha kuwa mshtakiwa alikuwa na notice ya kosa la uchochezi kwa vile ushahidi ulijikita huko. Hapa ndipo alipokosea, kwani upande wa utetezi uliandaa mashahidi na hoja zao kupinga UHAINI (kosa linalobeba adhabu ya kifo), na Lissu hakupewa nafasi mahsusi ya kisheria kujitetea dhidi ya viini (elements) vya KOSA JIPYA la UCHOCHEZI.
2. KUCHANGANYA "NIA YA KIHALIFU" (MENS REA).
Kesi ya Zombe inaeleza kuwa ili kosa dogo liweze kutumika, lazima viini vya kosa hilo viwe vimefanyiwa uchambuzi kamili wa kisheria ikiwemo nia ovu (mens rea) inayohusiana na kosa hilo.
KOSA LA JAJI: Katika maelezo yake ya awali, Jaji Ndunguru alisema kukubali kuwa maneno yalitamkwa hadharani (admission of words) si sawa na kukubali nia ya kihalifu (admission of criminal intent). Cha kushangaza, baadaye aligeuka (akala matapishi yake mwenyewe) na kutumia maneno HAYO HAYO kama ushahidi wa moja kwa moja kuwa Lissu alikuwa na nia ya kuchochea umma ili kuvuruga uchaguzi.
Hapa, mahakama ilishindwa kuchambua kwa kina muktadha wa kisiasa wa kauli hizo (ambazo Lissu alisema zililenga kudai mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi) na badala yake ikachukulia kuwa "kufanya uchochezi" kuwa ni sehemu ya uhaini.
3. TOFAUTI YA VIINI VYA MAKOSA (Cognate Offence).
Jaji Ndunguru ameshindwa kujiuliza, Je kosa la uchochezi chini ya kifungu cha 390 linaweza kuwa cognate offence (kosa linaloendana kirahisi) na kosa la uhaini?
Kesi ya Zombe inataka makosa hayo (UHAINI na UCHOCHEZI) yawe na uhusiano wa karibu sana KIVIINI. Uhaini unahusika na kuipindua au kuitishia mamlaka ya nchi/Serikali, wakati uchochezi uliotumika hapa ulidaiwa kulenga "kuvuruga uchaguzi".
Hapa, mahakama ililazimisha TAFSIRI POTOFU ili tu Lissu asiwe huru kabisa baada ya kuona shtaka kuu la uhaini limeshindwa kuthibitika.
Hizi hoja zitatumika kwenye rufaa na Lissu ana hoja kama 15 hivi kushinda rufaa isipokuwa kama Mahakama ya Rufani itakubali kula MATAPISHI yake yenyewe.
Ndugu zangu, hii ADHABU ni ya KISIASA na Lissu AMEONEWA wazi wazi. Sheria imekiukwa kwa 100%.
HAKI HAIOMBWI BALI HAKI HUPIGANIWA.
#BabaMwita ⚖️
Datius Faustine retweeted
TUWEKE REKODI SAWA:
Siku ya tarehe 6/11/2026, Wakili Msomi Tundu Antiphas Mughwai Lissu, Jeshi la mtu mmoja, AMEISHINDA CCM, Serikali & Mahakama huku akiwa AMEFUNGWA MIKONO kwa nyuma.
Datius Faustine retweeted
ADHABU YA LISSU NI YA KIMKAKATI:
Jaji ametoa miaka 4 kwa TAL pasipo kuzingatia KANUNI & MIONGOZO ya utoaji ADHABU! Kisheria, adhabu inapaswa kutolewa kwa kuzingatia sheria & miongozo. Huu ni UTARATIBU wa LAZIMA sio hiyari ya Jaji. Kanuni ambazo mahakama imekiuka KIMKAKATI:
1. KUKIUKWA KWA KIFUNGU CHA 172(2)(c) cha CPA (Siku 577 za Mahabusu).
Mahakama inapotoa adhabu ya kifungo, inapaswa KUZINGATIA (kupunguza) muda WOTE ambao mtuhumiwa alikaa gerezani au chini ya ulinzi kabla ya kukutwa na hatia. Msimamo huu ni wa kisheria na wa lazima chini ya Kifungu cha 172(2)(c) kikisomwa sambamba na Miongozo ya Utoaji Adhabu ya Mahakama (Tanzania Sentencing Guidelines 2023).
TAL alikaa mahabusu kwa jumla ya siku 577 kabla ya hukumu yake. Kisheria, siku hizi zilitakiwa kukatwa moja kwa moja kwenye miaka 4 (siku 1,461) na kumbakizia adhabu ya siku 884 anapoingia gerezani kutumikia kifungo siku ya kwanza.
2. KUFUMBIA MACHO MISIMAMO YA MAAMUZI (PRECEDENTS) ZA MAHAKAMA YA RUFANI.
Kwa kuacha kukata siku hizo 577, jopo la majaji 3 limekiuka kwa makusudi(kimkakati) misimamo thabiti ya kisheria iliyowekwa na Mahakama ya Rufani ya Tanzania (Court of Appeal), ambayo INALAZIMISHA mahakama za chini kukata muda wa mahabusu.
Baadhi ya kesi hizo ni: Godbless Simon vs Republic (Criminal Appeal No. 647 of 2022) [TZCA 355]: Ambapo Mahakama ya Rufani ilisisitiza kuwa kuacha kukata muda wa mahabusu ni ukiukwaji wa matakwa ya lazima ya Kifungu cha 172(2)(c) cha CPA, na ikalazimika kuingilia kati kupunguza adhabu ili kufidia muda huo uliosahaulika.
Pia, kesi ya Waziri Amani vs Republic: Ambapo Mahakama ya Rufani ilibainisha wazi kuwa kutohesabu muda tangu mshtakiwa alipokamatwa hadi siku ya hukumu kunafanya adhabu nzima kuwa na kasoro ya kisheria (illegal sentence).
3. HILA YA KUFUMBIA MACHO ADHABU YA FAINI (OPTION OF FINE).
Hapa kuna upotoshaji mkubwa zaidi wa kisheria na hila iliyofanywa na mahakama. Ikiwa sheria inayomtia hatiani TAL inatoa adhabu ya Faini AU Kifungo (Option of a Fine or Imprisonment), kanuni za kisheria na miongozo ya utoaji adhabu INALAZIMU Jaji kuipa kipaumbele faini kwanza, hususan kwa mkosaji aliyetiwa hatiani kwa MARA YA KWANZA (first offender).
👆🏽 Hili ni TAKWA LA LAZIMA la Miongozo ya Mahakama: Chini ya Miongozo ya Utoaji Adhabu ya Tanzania ya Mwaka 2023 (The Tanzania Sentencing Guidelines, 2023) [Kanuni ya 137 / Sehemu ya (i)], sheria inaelekeza wazi kuwa: "Pale ambapo kosa lina adhabu ya faini au kifungo, mkosaji wa mara ya kwanza anapaswa kupewa adhabu ya faini, isipokuwa tu kama kosa hilo ni la kikatili sana..."
Msimamo wa Kimahakama kuhusu suala hili (Precedents): Katika kesi maarufu ya Salum Shabani v. Republic [1985] TLR 71, Mahakama ilitamka wazi kuwa: "Ambapo Bunge limetoa hiyari ya faini au kifungo, mahakama inapolazimika kutoa adhabu LAZIMA ihakikishe kuwa adhabu ya faini inatolewa kwanza, na kifungo kinakuja tu pale mshitakiwa anaposhindwa kulipa faini hiyo (in default of payment)."
HILA ILIYOTUMIKA:
Jaji amefanya HILA kwa kufumbia macho kwa makusudi maelekezo ya kesi tajwa 👆🏽 & miongozo ya utoaji adhabu. Alijua fika kuwa TAL ana uwezo wa kulipa faini na wananchi wangemchangia ndani ya dakika chache. Ili kukwepa TAL asilipe faini na kubaki nje, Jaji aliruka kabisa hiyari ya faini na kumtwanga kifungo cha moja kwa moja cha miaka 4 gerezani bila sababu za msingi za kisheria zilizothibitishwa.
4. MPANGO WA KUZUIA DHAMANA WAKATI WA RUFAA (Bail Pending Appeal).
Hapa ndipo penye SIRI kubwa ya kimkakati ya ADHABU hii. Chini ya sheria za utaratibu wa makosa ya jinai, mahakama ina mamlaka ya kutoa dhamana kwa mfungwa anayesubiri rufaa yake isikilizwe (Bail Pending Appeal) pale tu kunapokuwa na sababu maalum (exceptional circumstances): ikiwemo hali ya afya, muda aliotumikia na uliobaki wa kifungo, sababu ambazo hulazimisha mahakama kutoa dhamana hii ni pamoja na ADHABU KUWA FUPI au MUDA MCHACHE WA KIFUNGO (Short Custodial Sentence), kwani kuna hatari adhabu ikaisha kabla ya rufaa kusikilizwa.
INAENDELEA 👇🏽
Datius Faustine retweeted
BAIL PENDING APPEAL:
Kwa kuwa TAL ameshinda kesi ya UHAINI ambayo haina dhamana, na kukutwa na hatia kwa kosa la UCHOCHEZI, Lissu anaweza kuwa nje kwa DHAMANA kupitia utaratibu unaojulikana kisheria "BAIL PENDING APPEAL" kwa sababu uchochezi una dhaminika, hata kama mtu amefungwa. Ila tu utaratibu ni kwamba, ni LAZIMA mfungwa aanze kutumikia kifungo chake gerezani japo kwa siku moja tu.
Hii inawezekana kama mawakili watajenga hoja za AFYA ya Lissu na kwamba atashindwa kupata matibabu stahiki akiwa gerezani. Pia, siku 577 alizokaa gerezani ni fimbo ya kuomba dhamana. Imefanyika mahakama Kuu & pia kuna msimamo wa mahakama ya Rufani juu ya utaratibu huu.
HAKI HAIOMBWI bali HUPIGANIWA.
Datius Faustine retweeted
Prof Tibaijuka aliniambia tuna kazi ngumu kuliko ya Mwl Nyerere.
Nyerere alipambana na wakoloni kwanza walikua wanafuata sheria.
Lakini hawa wakoloni weusi hawafuati sheria.
Wakaloni walikua hawatoi rushwa.
Wakoloni weusi wanahonga kila mtu.
Ukweli ni kwamba tutawashinda hata wakitumia nguvu gani.
Datius Faustine retweeted
Some family members of Chadema national chairman Tundu Lissu followed proceedings in his treason trial through social media as they mourned the death of his elder brother, Alute Mugwai Lissu.
Datius Faustine retweeted
Sijawahi ona watu wanasifu na kuabudu on the internet kama leo humu Twitter...things i love to see,nawasihi tuwe tunamtegemea Mungu kwenye kila kitu...sio hili la leo tu.
Datius Faustine retweeted
TUNDU LISSU ; Wakili Wa serikali amesema adhabu ya juu ni Kifungo cha miaka mitano au faini au Vyote viwili.
Datius Faustine retweeted
"Tafsiri ya maneno ya Lissu: tumeongozwa na kanuni kuwa nia ni internal state of mind. Lazima iambatane na ushahidi wa kimazingira na vitendo vya kufanya uhaini. Nia ovu siku zote inakuwa inferred kutoka kwa maneno na matendo ya mshtakiwa." - Mahakama Kuu 6.11.'26.
Datius Faustine retweeted
Ukiwa BABA wa familia pride yako ni kuhakikisha unaitunza na kuhudumia familia yako. Kusomesha na kutoa kodi ya meza peke yake HAITOSHI. Jitahidi sana kutenga muda kuzungumza na wanafamilia wakueleze yaliyo moyoni mwao na kutengeneza “moments” pamoja. Ubaba ni MAJUKUMU sio kende.
Datius Faustine retweeted
Exceptionally long night for us since independence. Good lucky, Idol. #FreeTunduLissu
Datius Faustine retweeted
After 40, everyone is being told to do more cardio, lift lighter and eat less.
I know this will upset some people.
It's the opposite of what works.
Here are the 4 mistakes to stop, and what to do instead:

























