Pinned Tweet
2 Timotheo 4:2
[2]lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.
LIVING GOSPEL: Mission and belief
Mr Stan retweeted
Warumi 5:1
Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,
The world will change. Tukiwa na waandishi wenye akili na maarifa kama wewe. Mungu atunze akili yako. Be blessed.
Kwa nini unaumia mwenzako akifurahi? Umewahi kujiuliza swali hilo? Kwa nini inakusumbua mtu akiishi maisha yake? Umeona mwenzio kaenda Marathon hata mia hajakuomba, unaigeuza agenda ya kumsimanga. Umekaa mahali na mtu anakueleza namna mambo yalivyomnyookea unahisi kama anatamba. Unasikia mwenzio anashuhudia kanisani vile Mungu amemtendea, amehitimu masomo, amepata usafiri, amepandishwa cheo, amepanua biashara, amesafiri ng’ambo ya nchi. Unachekea moyoni, ‘huyu naye!’ Watu hawa hawa wangesema wanavyoteseka na maisha pengine usingeona tatizo.
Siku hizi mitandao nayo, kwa namna fulani, inasaidia watu kusema mambo yanayotokea kwenye maisha yao. Wapo, kwa sababu mbalimbali, wataonesha wamekula nini, wanaishi vipi na wenzi wao, wanasafiri na kadhalika. Lakini pia ipo mitandao inayopendwa na wale wanaotangaza mikutano wanayohudhuria, nchi mpya wanazotembelea, kazi mpya wanazopata, mageuzi wanayoyasababisha, watu wakubwa wanaokutana nao na shughuli nyingine zinazoonesha uwezo wao wa kiakili, uzoefu wa kazi na kadhalika.
Sote, kwa viwango tofauti, tunajitambulisha na hali fulani zinazobeba tafsiri mbalimbali za kufanikiwa. Kuna mahali tunaenda, kuna kitu tunakihitaji, kuna hali tunatamani itokee na tukiipata tunajisikia watu wa maana. Hizi ni hisia za ufahari. Kila mwanadamu anazo hasa hitaji la kujiona kuna kitu ameweza linapotimilizwa. Tunatofautiana tu kitu gani kinachobeba kuweza kwetu lakini ni hakika hatupendi kujiona wanyonge. Ndio maana haishangazi tukipata chochote kinachotufanya tujione tumefanikiwa tunatamani (saa nyingine) na wengine wafahamu.
Kuna mtu akisafiri kwenda ng’ambo hawezi kunyamaza. Inamsaidia kujisikia fahari kuwa imetokea. Mwingine akipanda ndege atapiga picha airport na kuposti. Inampa hisia za ‘nimeweza.’ Unaweza kuona ushamba lakini kwake hiyo ni hatua muhimu kwenye maisha yake. Wakati wewe umevuka hatua ya kupiga picha kwenye kile ‘kidirisha’ lakini na wewe hunyamazi ukihudhuria mkutano na kukutana na wasomi wenzio. Mwingine akijenga ‘room mbili’ atatafuta namna aseme kahamia kwake. Kwake kujenga ni mafanikio makubwa hata kama wewe umeshavuka huko. Unaweza kumsema lakini hata wewe ukipata PhD, ukichapisha machapisho yako, ukapandishwa cheo hunyamazi.
Kutokuwaacha watu wafurahie maisha yao ni kujipa umuhimu usiokuwanao. Watu wanapambana kwa namna tofauti. Wengine wanatafuta D mbili mwaka wa tano sasa, wengine wanapambana wawe ma-Profesa. Wengine wanakomaa kuanzisha miradi, wengine wana ndoto ya kupanda ndege. Wengine wanatamani kukutana na mtu fulani maarufu, wengine wanapambana kuwa mamilionea. Kila mtu ana ndoto zake kwa hatua zake na zikitimia anatamani ‘kushuhudia’ kwa namna anayoona inafaa—mwingine WhatsApp Status, Instagram, Facebook, LinkedIn, Kanisani, kijiweni na kwingineko. Kutaka kujiona wewe ndio unastahili kujisikia fahari lakini mwenzio wawe wanyonge, waogope kufurahia kinachotokea kwenye maisha yao, hilo ni tatizo la kiburi. Kama hajakusimanga na kunyanyasa kwanini usimwache afurahie safari ya maisha yake?
Hausomi neno la Mungu, kutafakari wala kuchambua maandiko na unategemea kuelewa sauti ya Mungu. Mungu hawezi kuzungumza na wewe kama humwelewi. Mara nyingi sana Mungu amejaribu kuongea na watu lakini hawakumwelewa. Kaa katika maarifa ya neno utamwelewa Mungu (Zab 119:130)
Ulimwengu wa roho ni kama akili ndani ya ubongo, ingawa akili haionekani lakini matokeo yake yanaonekana. Magari, ndege, pikipiki hivyo vyote ni matokeo ya akili. Vivyo hivyo ulimwengu wa roho huamua matokeo ya maisha ya watu hata ingawa hauonekani kwa macho ya nyama.
Yesu alisema kulikuwa na wakoma wengi katika siku za Elisha, lakini aliyeponywa ni Naamani pekee (mgeni), kwa neno la binti wa kazi aliamini na kufata muujiza. Siku moja ukiamka na kuacha kumdharau mchungaji wako, usiyaone mahubri yake kama kelele, Mungu atakuponya kirahisi sana.
Ni jambo zuri kuombea moyo wako kuliko pesa na uchumi. Maana moyo mzuri humvuta BWANA akupe vyote. Moyo mzuri hutengeneza Moyo wa ibada ambao utakupa neema ya kutafuta ufalme wa Mungu, na hapo kanuni ya Mungu itakuinua na kukubeba sawa sawa na neno lake (Mt. 6:33).







