Mnada Nchege 623/2026 (@mnadanchege) header
Mnada Nchege 623/2026 (@mnadanchege) profile picture

Mkulima

Mwanza, Tanzania
Joined March 2014
Photo by Mnada Nchege 623/2026 (@mnadanchege)Photo by Mnada Nchege 623/2026 (@mnadanchege)Photo by Mnada Nchege 623/2026 (@mnadanchege)Photo by Mnada Nchege 623/2026 (@mnadanchege)Photo by Mnada Nchege 623/2026 (@mnadanchege)Photo by Mnada Nchege 623/2026 (@mnadanchege)Photo by Mnada Nchege 623/2026 (@mnadanchege)Photo by Mnada Nchege 623/2026 (@mnadanchege)Photo by Mnada Nchege 623/2026 (@mnadanchege)Photo by Mnada Nchege 623/2026 (@mnadanchege)
Ile maana ya kukinukisha tafsiri yake ndio hii ona anavonuka kimataifa. Lisu akili kubwa sana katumia akili kampanikisha mama wa watu kajaa 18 zake yeye na watu wake wanacheza beats la Lisu
8
18
265
22,922
Mnada Nchege 623/2026 retweeted
TUTASHINDA……….
21
81
3
452
7,195
Mnada Nchege 623/2026 retweeted
KARIBUNI TUJADILI HUKUMU YA YESU: Njooni tujadili HUKUMU YA YESU na TUMCHAMBE PILATO kwa KUSHINDWA KUTENDA HAKI👇
13
60
4
199
6,420
Mnada Nchege 623/2026 retweeted
KUHUSU UONGO WA AHMAD MAKELE: Leo tarehe 26 Novemba 2026 nimeliambia BARAZA LA ELIMU YA SHERIA chini ya Mwenyekiti wake Jaji MUSTAPHER SIYANI, kwamba; AHMED ABDULRAHMAN MAKELE, ni MUONGO kwa kuwa, kwa KIAPO chake hapo 👇 amesema yeye ni WAKILI na MKURUGENZI WA TLS.😂😂
7
21
109
6,186
Dadekiiii, Nchi imevimba……. Watanzania kila mmoja wetu akijitoa kutetea na kudai haki kama hivi basi TUTASHINDA HII VITA DHIDI YA WAUWAJI WANAOSHIKILIA NCHI KWA KUTUMIA JESHI LA POLISI……. Kama uko Tz na huwezi kujitoa kwa jina lako basi anzisha page anonymous ya kudai haki kwenye mitandao ya Instagram, tiktok na Facebook. Kama uko nje ya Tanzania tafadhali tumia jina lako na sura yako mwenyewe, account zenye mtu anaonyesha sura yake ndio zinashawishi wananchi kiurahisi zaidi kuliko account zisizo na mtu anaejulikana. Nawaomba haswa diaspora wote tuwe wanaharakati tunaoweka sura zetu kwenye page. Hii ndio njia effective tunaweza kuwasaidia wenzetu nyumbani wapate uhuru wao kutoka kwa WAKOLONI WEUSI!!!! WAKOLONI WEUSI NI WAKATILI KWA WATANZANIA KULIKO WAKOLONI WEUPE WALIVYOKUWA WAKATILI KWA KINA NYERERE….
25
393
5
2,760
158,173
Mnada Nchege 623/2026 retweeted
Mwenyekiti wetu Tundu Lissu amezishinda risasi 32 za ccm na dola.. Walitaka kumuua mwaka 2017 wakashindwa. Wamejaribu kumnyonga kwa kesi ya uhaini wa uongo wameshindwa. Wamemfunga kwa uchochezi wa uongo. Makaburu hawakuwahi kumpiga risasi Mandela wala kumuondolea ubunge wake. Wamlimfunga tu kwa mda mrefu na baadae alitoka. Historia ya Mwenyekiti Lissu itaandikwa kwa wino wa dhahabu, sio Raila wala Mandela amefanyiwa unyama na serikali kama ambao Mwenyekiti Lissu amefanyiwa na anaendelea kufanyiwa. Tutashinda na tutavuka.
56
448
8
1,800
31,689
Mnada Nchege 623/2026 retweeted
WATU WANAJADILI HUKUMU YA YESU NA HAWAKUWEPO KWA PILATO: Jaji Mkuu GEORGE MASAJU anapaswa kufahamu kwamba; WATU WANAJADILI HUKUMU YA YESU NA HAWAKUWEPO MAHAKAMANI, LAKINI WANAMLAUMU PILATO. Kwa hiyo, kujadili HUKUMU YA TUNDU LISSU, siyo KOSA.😂😂
33
140
1
647
16,269
Mnada Nchege 623/2026 retweeted
Jaji mkuu Masaju Watanzania wa sasa sio wajinga. Hukumu ya haki haifanyiwi kampeini wala haihitaji utetezi wako, hukumu ya haki inajitetea yenyewe.
42
420
9
1,565
26,873
Mnada Nchege 623/2026 retweeted
Hakuna wa kuja kutuokoa Si Lissu, si Mange, si mimi si mwanaharakati yoyote! Si Marekani, EU, nchi yoyote Si UN, ICC ama shirika yoyote You get the government you deserve! Ukikubali kudharauliwa, kukandamizwa na kikundi kidogo na kuogopa kuRESIST - basi utaishi ktk dhulma Ndo ukweli mchungu #TutaelewanaTu
29
233
8
969
80,869
Mnada Nchege 623/2026 retweeted
HAWA WAHUNI WANALIPWA NA KUWEZESHWA KUFANYA UCHAFU HUU! Kwa nini tunaendelea kuzunguka bila kuchukua hatua ya msingi? Kwa nini tusianzishe Tume Huru ya Uchunguzi au kuruhusu Wachunguzi Huru kuchunguza ukweli wa mambo? Wanaogopa nini? Kuna kitu gani wanachohofia kisichojulikana? Kama kweli hatuna kosa la kuficha, kwa nini tukimbilie MARIDHIANO yasiyo na UKWELI, HAKI NA UWAJIBIKAJI? Ukweli haupaswi kuogopwa, na uwajibikaji haupaswi kukwepwa. Mimi si mgeni katika nchi hii. Ninafahamu kinachoendelea. Ninafahamu kwamba kuna watu wanaolipwa kwa kazi maalumu ya kutuchafua, kuwaharibia wengine majina na hata kuwezeshwa kutafuta roho zetu. Haya si mambo yanayopaswa kupuuzwa wala kufunikwa kwa kauli za maridhiano. Tunachodai ni rahisi TUME HURU, YA KUAMINIKA NA ISIYO NA UPENDELEO.Tume itakayochunguza, kubaini ukweli na kuweka msingi wa haki na uwajibikaji. Hakuna maridhiano ya kweli bila ukweli. Hakuna amani ya kudumu bila haki. Na hakuna taifa linaloweza kupona kwa kuficha maovu na kukwepa uwajibikaji. ENGLISH VERSION THESE RUFFIANS ARE BEING PAID AND FACILITATED TO CARRY OUT THIS DIRTY WORK!** Why do we keep going round in circles instead of taking the most fundamental step? Why don't we establish an Independent Commission of Inquiry or allow independent investigators to investigate and establish the truth? What are they afraid of? What is it that they do not want uncovered? If we genuinely have nothing to hide, why should we rush into RECONCILIATION without TRUTH, JUSTICE AND ACCOUNTABILITY? Truth should never be feared, and accountability should never be evaded. I am no stranger to this country. I know what is happening. I am aware that there are individuals allegedly being paid to smear our names, damage the reputations of others, and even facilitate efforts to threaten our lives. These are serious matters that must not be ignored, trivialised or concealed behind the rhetoric of reconciliation. Our demand is simple AN INDEPENDENT, CREDIBLE AND IMPARTIAL COMMISSION OF INQUIRY.  A commission mandated to investigate, establish the truth and lay the foundation for justice and accountability. There can be no genuine reconciliation without truth. There can be no lasting peace without justice. And no nation can heal by concealing wrongdoing and evading accountability. TRUTH, JUSTICE AND ACCOUNTABILITY WILL HEAL THE NATION. BAK MWABUKUSI
45
144
5
476
35,732
Mnada Nchege 623/2026 retweeted
House Negro (ccm) wanafurahia mabaki ya majambazi wanaoteketeza Nchi.
17
185
7
783
18,446
Mnada Nchege 623/2026 retweeted
Tenga dakika zako 9 MSIKILIZE BONGO ZOZO. Repost 200
49
695
7
2,888
133,767
Mnada Nchege 623/2026 retweeted
PUMZIKA KWA AMANI, BINTI. Kwa masikitiko makubwa na huzuni isiyoelezeka, tunakuaga wewe uliyeondoka duniani kabla ya wakati wako. Uhai wako umekatishwa kikatili na watu wazima waliopoteza utu, huruma na thamani ya uhai wa binadamu. Inasikitisha zaidi kusikia kwamba, licha ya vifo na maumivu ya wahanga, bado kuna wanaokimbilia kuendeleza kile wanachokiita MARIDHIANO, kana kwamba wamesahau kwamba UKWELI, HAKI NA UWAJIBIKAJI NDIO MSINGI WA MARIDHIANO YA KWELI NA YA KUDUMU. Binti, kifo chako hakitakuwa sababu ya sisi kunyamaza. Tutaendelea kudai na kupigania haki yako na haki ya wahanga wengine wote. Hatutakubali damu iliyomwagika, maisha yaliyopotea na machozi ya familia zilizofikwa na majonzi vifunikwe kwa pazia la maridhiano yasiyo na ukweli, haki wala uwajibikaji. MARIDHIANO SIYO KICHaka CHA KUJIFICHA KUKWEPA UWAJIBIKAJI. Hatuwezi kujenga amani ya kweli kwa kusahau waliopoteza maisha yao wala kwa kuwanyima wahanga haki wanayostahili. Pole sana kwa familia, ndugu, jamaa na wote walioguswa na msiba huu mzito. Hakuna maneno yanayoweza kufuta maumivu yenu. Tunawaombea nguvu, faraja na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu. PUMZIKA KWA AMANI, BINTI. HAKI YAKO TUTAENDELEA KUIDAI. KUMBUKUMBU YAKO HAITAFUTIKA. ××××××××××××××××××××× REST IN ETERNAL PEACE, DEAR DAUGHTER. With profound sorrow and indescribable grief, we mourn your untimely departure from this world. Your life was cruelly cut short by adults who appear to have lost their humanity, compassion and respect for the sanctity of human life. What makes this tragedy even more heartbreaking is hearing that, despite the deaths, suffering and anguish of victims and their families, some are still determined to proceed with what they call RECONCILIATION, as though they have forgotten that TRUTH, JUSTICE AND ACCOUNTABILITY ARE THE VERY FOUNDATION OF GENUINE AND LASTING RECONCILIATION. Our beloved daughter, your death will not silence our voices. We shall continue to demand and fight for justice for you and all other victims. We shall not allow the blood that has been shed, the lives that have been lost and the tears of grieving families to be buried beneath a false veil of reconciliation that has neither truth, justice nor accountability. RECONCILIATION MUST NEVER BECOME A SANCTUARY FOR THOSE SEEKING TO EVADE ACCOUNTABILITY. There can be no genuine and lasting peace built upon forgotten lives, suppressed truths and denied justice. My deepest condolences go to your family, relatives, loved ones and everyone affected by this heartbreaking loss. REST IN ETERNAL PEACE. WE SHALL CONTINUE TO DEMAND JUSTICE FOR YOU. YOUR MEMORY SHALL NEVER BE ERASED. BAK MWABUKUSI
43
315
2
1,252
18,671
Mnada Nchege 623/2026 retweeted
MARIDHIANO AU UPATANISHO HAVIWEZI KUFANIKIWA BILA UKWELI, HAKI NA UWAJIBIKAJI! Maridhiano au upatanisho wa kweli na wa kudumu hauwezi kufanyika bila kwanza kuwepo kwa Tume Huru, Jumuishi na Yenye Kuaminika ya UKWELI, HAKI NA UWAJIBIKAJI. Tume hiyo lazima ijumuishwe na wataalamu wenye uwezo na uadilifu kutoka ndani na nje ya nchi, pamoja na uwakilishi wa wahanga wenyewe, ili ukweli wote kuhusu yaliyotokea uweze kubainika, haki itendeke na uwajibikaji uweze kupatikana. Hatuwezi kwa dhati kufikiria kukaa kwenye meza ya mazungumzo huku wanaharakati, watetezi wa haki za binadamu na wanasiasa wanaosimamia misingi ya UKWELI, HAKI NA UWAJIBIKAJI wakiendelea kuwindwa, kutishwa, kuwekwa kizuizini au kubambikiwa makosa yasiyo na dhamana kwa hila bila aibu halafu hao hao wanaofanya unyama huo wanahubiri Nuru katikati ya Giza. Hali inakuwa ya kusikitisha zaidi pale ambapo kiongozi mkuu wa chama kikuu cha upinzani ndugu Tundu Antipas Lissu kwa Uonevu na ukatili usiomitjilika  anapokuwa gerezani katika mazingira ambayo uhalali na uadilifu wake wa kisheria vinazua maswali mazito. Ni muhimu tuelewe jambo moja na Tuliseme bila kupepesa macho: Mgogoro huu si mgogoro wa vyama vya siasa; ni mgogoro unaohusu haki, utu, usalama na uhai wa RAIA. Kwa hiyo, tuache kujidanganya, kujilisha upepo au kubeza na kupuuza madhila ya wahanga, hususan vifo na mauaji yanayodaiwa kufanyika dhidi ya raia wasio na hatia kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa tarehe 29 Oktoba 2025. Maumivu ya wahanga hayawezi kufutwa kwa matamko ya kisiasa, wala ukweli hauwezi kufunikwa kwa kauli za maridhiano. Maridhiano si njia ya kufuta makosa, kuficha ukweli, kusamehe bila kujua kilichotokea au kuwapa kinga wale wanaopaswa kuwajibika. Maridhiano ya kweli yanapaswa kujengwa juu ya kukiri ukweli, kutambua madhara, kutenda haki, kurejesha utu na kuhakikisha uwajibikaji. Huwezi kujenga amani ya kudumu juu ya misingi ya dhuluma, ukimya na kutokuwajibika UKWELI ndio mwanzo. HAKI ndiyo msingi. UWAJIBIKAJI ndiyo daraja. MARIDHIANO ndiyo matokeo. Kufanya kinyume na utaratibu huu si kujenga maridhiano; ni kudhihaki ufahamu wetu, kupuuza maumivu ya wahanga na kuahirisha mgogoro ambao hatimaye utahitaji kutatuliwa. BAK MWABUKUSI UKWELI, HAKI NA UWAJIBIKAJI VITALIPONYA TAIFA
40
324
3
960
15,581
Mnada Nchege 623/2026 retweeted
Thank you @TheEconomist 👏🏽 #Tanzania is truly a deplorable state under Samia Suluhu! These treason trials spreading across the continent are SHAMEFUL! But what Suluhu is doing to Tundu Lissu is cowardly and extraordinarily evil! #FreeTunduLissu
6
96
220
10,489
WATANZANIA, tusikubali AFCON ikawapa ushindi wauwaji wa OCTOBER 29. TUHAKIKISHE afcon inaonyesha dunia kilichotokea Tanzania OCTOBER 29 2025…. NA KWAMBA TUNAJITAJI MSAADA WAO………
52
336
4
1,922
76,587
Wauwaji wanataka kupitisha katiba iliyopendekezwa na CCM 2015 kwenye ile tume ya katiba mpya……. Samia, Kikwete, Wambura, Mombo na Haji Othman (Chief of staff jeshi la wananchi) wanataka kujimilikisha nchi for the next 15 years.
130
487
13
2,726
294,155
Kimenukaaaaaaaaa…… Naingia kulala, nikiamka napeleka watoto shule alafu nawashushia video saa 3 usiku muda wa TZ….. Issue ni dipu kuliko…..:::
132
381
20
3,022
237,057
Mnada Nchege 623/2026 retweeted
‼️JAJI NDUGURU HAKUAZIMISHWA, ALISHIRIKI KWA HIARI KUANDIKA HUKUMU‼️ Taarifa niliyopata ni kuwa Jaji Ndunguru alizunguka kuulizauliza kuhusu cognate offense (yaani kosa dogo) la uhaini. Aling’ang’ania kuwa South Africa treason yaani uhaini Ina makosa madogo. Kwa SA ni kweli kosa linaendana na sedition na incitement lakini aliambiwa na kila aliyemwuliza kuwa kwa Tanzania hakuna kitu kama hiki. Akagoma kusikiliza sasa KAUMBUKA! 🙄 Sasa shida yeye ni mwenyekiti wa jopo na shida kubwa kwa sasa Tanzania hamna dissenting opinion, la sivyo hivyo kuna jaji au majaji wangeweka hukumu tofauti. Na ndiyo maana hukumu zilikuwa mbili. Ile inayomwonyesha Ndunguru peke yake ilivuja kabla ya kupandishwa Tanzilii, ilikuwa ni ya mfumo wa ndani wa mahakama. Hiyo ndo ilikuwa nakala yake aliyotii maelekezo ya Abdul! Ila uzuri Haki itashinda na washiriki wote wa dhulma watajulikana na kuwajibishwa! #FreeTunduLissu
61
257
11
1,269
122,944
Tunaelekea kwenye ushindi wa haki kwenye nchi yetu. Don’t take your foot off the gas…
35
292
1
1,840
95,996
Mnada Nchege 623/2026 retweeted
PAUL CHACHA, CCM ILISHAMFUKUZA NCHIMBI, KWA NINI BADO UNAMFUATAFUATA? Nimemsikia Paul Chacha jana akisema kwamba nilipokuwa CCM, kazi yangu ilikuwa kushika simu za Dkt. Emmanuel Nchimbi. Nataka kuweka mambo mawili wazi. Kwanza, sijawahi kuwa mbeba simu za Dkt. Emmanuel Nchimbi. Huo si ukweli. Pili, hata kama ningekuwa nafanya kazi hiyo, nisingeona aibu. Hakuna kazi halali inayomvunjia mtu heshima. Kinachomvunjia mtu heshima ni kusema jambo lisilo la kweli kwa lengo la kumdhalilisha mwingine. Lakini kuna jambo kubwa zaidi ambalo linanishangaza. Paul Chacha, CCM ilishamfukuza Dkt. Emmanuel Nchimbi. Kwa nini bado unaendelea kumfuatafuata? Mlimwondoa kwenye chama chenu. Ameondoka katika uongozi wa Serikali. Ametangaza kustaafu siasa. Sasa kila mnapotaka kunishambulia mimi, kwa nini lazima jina la Nchimbi lihusishwe? Kama una jambo dhidi yangu, sema kuhusu mimi. Kwa nini unahitaji kumvuta mtu mwingine ambaye hata hayupo kwenye mjadala wetu? Je, tatizo ni mimi, au bado kuna jambo kuhusu Nchimbi ambalo hamjalimaliza? Mimi simsemei Dkt. Nchimbi, wala sihitaji kujificha nyuma yake. Nina historia yangu, maamuzi yangu na wajibu wangu mwenyewe. Nilipokuwa CCM nilifanya kazi za kisiasa. Nilipoona siwezi kuendelea kusimama na mambo ambayo dhamiri yangu haikubaliani nayo, niliondoka. Nimewajibika kwa kauli na matendo yangu, na nimeomba msamaha hadharani. Lakini kuomba msamaha hakumaanishi nimepoteza haki ya kujitetea dhidi ya uongo. Paul Chacha, kuna tofauti kati ya kumkosoa mtu na kuendelea kumhusisha mtu mwingine katika kila shambulizi. CCM inaweza kumfukuza mtu kwenye chama, lakini haiwezi kufuta historia yake, utu wake wala haki yake ya kuheshimiwa. Na kama kweli tunataka kufanya siasa zenye maana, tujadili masuala yanayogusa maisha ya Watanzania. Tujadili Katiba Mpya. Tujadili uhuru wa Mahakama. Tujadili haki za wananchi. Tujadili mipaka kati ya chama tawala, Serikali na vyombo vya dola. Na zaidi, ningependa Paul Chacha atueleze kauli yake kwamba vyombo vya ulinzi na usalama ni mali ya CCM. Hilo ni suala kubwa kuliko madai ya nani alishika simu ya nani. Mwisho, Paul Chacha, unaweza kuendelea kunizungumzia mimi. Hiyo ni haki yako. Lakini usitumie jina la Dkt. Nchimbi kama silaha ya kunishambulia. Kama CCM iliamua kuachana naye, basi heshimuni uamuzi wenu wenyewe. Mimi sina tatizo kujadili historia yangu, lakini sitakubali historia yangu iandikwe kwa uongo. Na kumbuka: Kumwondoa mtu kwenye nafasi ni jambo moja; kuendelea kupambana na kivuli chake ni jambo jingine kabisa
8
37
1
288
24,136