mobappdev retweeted
Huwaga nashangaa sana mtu anapojiona yupo salama TANZANIA.
Kila siku nasemaga "KILA MTU ATAFIKIWA TUU NA UTEKAJI NI SUALA LA MUDA TUU".
Sasa tutegemee MADEREVA kugoma tena nchi nzima baada ya siku 3 kwasababu ya UTEKAJI unaoendelea nchini.
Na hawa wakigoma nadhani kila mtu anajua mziki wake. Hii ndio njia mliyochagua kuendesha nchi sio?
Tutafika tuu..!
ASANTENI MADEREVA UJUMBE UMEFIKA.
REPOST 200
mobappdev retweeted
"Kama tutaendelea kuwa IGP; ambaye vijana wake walifyatua risasi dhidi ya raia wasio na risasi, kama hatawajibika, hakuna kusonga mbele."
Kiongozi Mstaafu wa @ACTwazalendo
@zittokabwe
#Ukweli #Haki #Uwajibikaji
mobappdev retweeted
“Mauaji ya Oktoba 29, 2025 hayakuwa bahati mbaya, yalipangwa…”-; Sheikh
#Mo29 #TanzaniaMassacre
mobappdev retweeted
OCTOBER 29 - MWAKA MMOJA BAADA YA MAUAJI HATUWEZI KUSAHAU, HATUPASWI KUZOEA.
Leo, mwaka mmoja umetimia tangu matukio ya umwagaji damu ya Oktoba 29. Mwaka mmoja wa majonzi, maswali, majeraha ya mioyo na kumbukumbu za maisha yaliyopotea.
Tunawakumbuka waliopoteza maisha, tunazifikiria familia zilizopoteza wapendwa wao, na tunaitaka dhamiri ya taifa kutafakari kwa kina kuhusu thamani ya uhai wa binadamu.
Hatari kubwa kwa jamii si maovu yanapotokea pekee, bali ni pale jamii inapofikia hatua ya kuyazoea. Siku tunapoacha kushtushwa na kupotea kwa maisha ya watu, tunakuwa tumepoteza sehemu muhimu ya ubinadamu wetu.
Oktoba 29 isiwe tarehe ya kumbukumbu pekee. Iwe siku ya kutafakari, kutafuta ukweli, kudai haki na kuhakikisha kwamba misiba ya namna hii haijirudii.
Taifa haliwezi kujenga amani ya kudumu kwa kusahau maumivu ya wananchi wake. Amani ya kweli hujengwa juu ya ukweli, haki, uwajibikaji na heshima kwa uhai wa kila mtu.
Hatukumbuki kwa sababu tunataka kulipiza kisasi. Tunakumbuka kwa sababu tunataka haki, utu na taifa ambalo maisha ya kila Mtanzania yana thamani.
Oktoba 29. Hatutasahau. Hatutazoea. Haki na utu lazima vitangulie.
Wanataka maridhiano sio kubadili yaliyopita bali kuendelea kutawala yanayokuja
Kuridhiana na mtu anayewateka maelfu na kuwaua,ameua maelfu apate kutawala hali yakuwa amekataliwa
Kwahiyo tukamuombe aache kututeka na kutuua?
Kwahiyo tukampe uhalali wa mauaji aliyoyafanya?
mobappdev retweeted
HAKI YA TUNDU LISSU KUSIKILIZWA KIKAMILIFU:
Kwa kuwa MAHAKAMA KUU YA TANZANIA tayari imetamka kwamba; ilikuwa ni MAKOSA kwa Magereza KUMNYIMA Tundu Lissu, HAKI YA FARAGHA NA MAWAKILI WAKE, maana yake ni kwamba; HAKUSIKILIZWA KIKAMILIFU. Yote yajayo yatakuwa ni BATILI.
mobappdev retweeted
"Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga."
mobappdev retweeted
Majina 659 ya waliofariki 29 Oktoba, 2025.
Kama mtu unayemfahamu hayupo, muongeze hapo chini.
mobappdev retweeted
Huyu ndiye muumini halisi wa UISLAM achana na wale wazee wa ubwabwa...
Asante sana Mufti.
mobappdev retweeted
Replying to @Jambotv_
Hakika shekhe umezungumza kwa busara na hekima ya hali ya juu. Wenye kusikia wamesikia, wenye kushupaza shingo waache waadhibiwe na Allah.
mobappdev retweeted
Replying to @Jambotv_
Kama ya Mashehk wachache sana WALIONYOOKA ‼️... Allah bless you sheikh
VIDEO:
Mjumbe wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Aboubakar Mgodo ametoa mwito wa kuwa wakweli, kuwajibika ili kuponya majeraha na maumivu yanayowakabili wananchi waliopoteza ndugu na waliotoweka wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu.
Sheikh Mgodo ameyasema hayo leo, Oktoba 29, 2026, mkoani Dar es Salaam wakati wa Ibada maalum ya kuwakumbuka waliopoteza maisha, waliopotea, pamoja na majeruhi wa matukio ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa Oktoba 29, 2025.
“Uongo hauwezi kutufikisha pazuri. Tunashauri vyombo vyetu, serikali yetu tuwe wakweli. Kosa linaweza kutokea iwe kwa bahati mbaya au makusudi, lakini baada ya kosa watu wanatakiwa wajirudi”, ameeleza Sheikh Mgodo.
mobappdev retweeted
Leo umetimia mwaka mmoja tangu mauaji yaliyofanywa kwa makusudi na vyombo vya dola vya Tanzania dhidi ya Watanzania wasio na hatia.
Mauaji ya October 2025 yalikua yanaweza kuepukika na uchaguzi ukafanyika kwa amani na usalama.
Kwasababu ya kiburi na uchu wa madaraka watawala waliamua kupuuza wito wa mda mrefu wa viongozi wa dini, vyama vya siasa, mashirika yasiyo ya kiserikali na hata watu maarufu ya kutaka mabadiliko ya katiba na sheria za uchaguzi ili kuwezesha uchaguzi huru na haki.
Mpaka sasa mwaka mmoja baadae Nchi iko kwenye mkwamo mkubwa wa kisiasa, watu wanaendelea kutekwa, kuuawawa na kupotezwa.
Kila anaetoa sauti ya kukemea uovu na kutaka maridhiano na uwajibikaji wa kweli anakabiliwa na kifo au mashitaka ya uongo.
Inaonekana hawa watawala wameshindwa kujifunza kwa yale mabaya yaliyotokea, Inaonekana wanafurahia kuendeleza utawala wa mkono wa chuma, udikteta na ubabe, mauaji, utekaji na kunyamazisha badala ya kushawishi na kutatua matatizo.
Kwa kutumia njia hizi mbele ni giza tupu, hakuna sehemu ambayo utawala wa kibabe Umefanikiwa kunyamazisha watu wote, Nchi hii ina watu zaidi ya milioni 70, hakuna siku watu wote hawa watanyamazishwa kwa uongo na kikundi kidogo cha watu kwa kutumia ubabe.
Njia pekee ya kutatua mkwamo huu ni.
1. Kumuachia Mwenyekiti Lissu na kufuta kesi za uongo dhidi ya wanachama wetu wote.
2. Kuachia mateka wote na kusitisha utekaji na mauaji ya kiholela.
3. Kuruhusu msuluhishi huru (mediator) kuleta watu pamoja na kuzungumza kwa ukweli na uwazi.
4.Uwajibikaji bila upendeleo kwa wahusika wa mauaji, kulipa fidia familia za wahanga, kutibu majeruhi wote na kuwapa fidia.
5. Kuruhusu Uchunguzi huru na kuomba radhi mbele ya Watanzania kwa makosa makubwa yaliyofanywa na vyombo vya dola dhidi ya raia wake.
6. Kuandika katiba mpya ya Nchi na sheria za uchaguzi ambazo zitarudisha umoja na haki kwa kila mtu.
7. Kutamka kwa uwazi kwamba makosa kama yale hayatajirudia tena kwenye Nchi yetu.
8. Kuhakikisha familia zinapata miili ya wapendwa wao na kufanya maziko ya heshima, kiafrika na kidini.
Kuendelea kutumia ubabe ni kuchochea chuki, uhasama na visasi kwa siku zinajazo…
Watawala badala ya kutumia chawa na ubabe kujaribu kuhujumu Chadema na uongozi wa Chadema, Tumia busara kufanya jambo sahihi la kuponya Nchi hii.
Tunajua mipango yenu dhidi yetu, lakini haki haijawahi kushindwa.
Endeleeni kupumzika kwa amani wote mliouwawa kikatili na kibabe, poleni majeruhi na wahanga wote.
Haki inaweza kuchelewa Lakini haki itapatikana tu.
mobappdev retweeted
Kutaka kuweka tozo nyingine ya barabara ni wizi wa wazi wazi. Tayari Watanzania wanalipa kodi ya barabara kila wanaponunua mafuta. Huyo aitwaye Waziri wa Ujenzi au jina lolote lile la Wizara hiyo ajue hilo. Kwa wastani Mtu Mwenye gari ya uwezo wa CC 2500 kwa mwaka analipa si chini ya shilingi milioni mbili hadi tatu za Kodi ya kutumia Barbara. Shida hapa si malipo ya fedha bali matumizi yake kwani falsafa ya waliotwaa madaraka kwa kumwaga damu ya maelfu ya Watanzania ni "kula Kwa urefu wa kba zao". Sasa hapo kutakuwepo fedha za kujenga barabara?
mobappdev retweeted
Breaking 🚨 A very dangerous attack on Netanyahu in Tel Aviv it appears he has sustained severe injuries, and an aircraft is being dispatched to transport him to the United States. This is clearly evident from the footage. Don't remove my video X Twitter
Readers added context they thought people might want to know
Claims of a dangerous attack on Netanyahu in Tel Aviv with severe injuries are false; no such event is reported by credible media, and the video shows a 2013 attack on Bulgarian politician Ahmed Dogan.
english.factcrescendo.com/2026/04/13/201…
theguardian.com/world/benjamin…
timesofisrael.com/netanyahu-desp…
srilanka.factcrescendo.com/english/no-net…




















